Orodha ya Viumbe vya Visasili
Viumbe vya visasili ni viumbe vyenye nafasi katika visasili vya mataifa na tamaduni mbalimbali. Mara nyingi ni watu wenye tabia za ajabu au mapepo ya watu, wanyama wenye tabia za ajabu au pia viumbe ambao ni mchanganyiko wa binadamu na wanyama.
A
haririAfriti (Uarabu) Jini wa moto
Alseidi (Ugiriki) Nimfa wa viunga
Auloniadi (Ugiriki) Nimfa wa malisho
B
haririBanshi (Eire) Pepo wa kifo
Behemothi (Uyahudi) Kiboko mkubwa kabisa wa Biblia
C
haririChenjilingi (Ulaya) Mtoto asiye binadamu (kizimwi, elfi, troli) aliyebadilka kwa mtoto wa binadamu aliyetekwa.
D
haririDhampiri (Balkani) Nusu binadamu na nusu vampiri
Dragoni (Duniani kote)
Driadi (Ugiriki) Nimfa wa miti
Dubwana (Duniani kote) Kiumbe cho chote chenye kutisha cha visasili kama: Mumiani, Jitu, Joka na kadhalika.
E
haririElfi (Ujerumani) Pepo wa rutuba
F
haririFahali wa Krete (Ugiriki) Fahali wa kuogofya
Farasi wa Diomede (Ugiriki) Farasi alaye binadamu
Finiksi (Ufinisia) Ndege wa moto
Furia (Ugiriki) Zimwi wa kisasi au haki wenye mabawa.
G
haririGargulya (Ufaransa) Joka wa maji
Gorgona (Ugiriki) Wanawake wenye nyoka kama nywele
Grifoni (Ugiriki) Mvyauso wa simba na tai
H
haririHamadriadi (Ugiriki) Nimfa wa waloni
Harpia (Ugiriki) Pepo wa kike wenye mwili wa ndege na kichwa cha mwanamke
Hekatonkheire (Ugiriki) Majitu yenye mikono 100 na vichwa 50
Hesperidi (Ugiriki) Nimfa wa jioni
Hiadi (Ugiriki) Nimfa wa mvua
Hipokampo (Ugiriki na Ufinisia) Mvyauso wa farasi na samaki
I
haririInkubi (Ulaya) Shetani dume wa usiku abakaye wanawake katika jinamizi
J
haririJini (Uarabu) Pepo wenye atimizaye matakwa
Jitu (mitholojia) Mtu mkubwa sana
Joka (Duniani kote) Nyoka mkubwa
K
haririKambioni (Ulaya) Mvyauso wa binadamu na inkubi au sukubi
Khimaira (Ugiriki) Mvyauso wa simba, mbuzi na nyoka
Kibeti (Ujerumani) Pepo mdogo
Kibwengo (Uswahili) Pepo wa bahari au miti
Kinyamkela (Uswahili) Zimwi wa upepo
Kitu nusi (Uswahili) Pepo wa bahari watufatao damu
Kizimwi (Duniani kote) Zimwi wadogo wenye mabawa
Kokatriksi (Ulaya) Mvyauso wa kuku na mjusi
Koma (Uswahili) Roho wa marehemu
Kulungu wa Kerineya (Ugiriki) Kulungu wa jike wenye pembe za dhahabu na makwato ya shaba
L
haririLeprekoni (Eire) Pepo aliye na chunga cha dhahabu mwishoni mwa upinde wa mvua
Leviathani (Uyahudi) Mamba mkubwa wa bahari wa Biblia
Lilithu (Mesopotamia) Shetani wa kike mwenye mabawa
M
haririMalaika (Ukristo, Uyahudi na Uislamu) Kuwa wa mbinguni wenye mabawa
Mantikora (Uajemi) Mvyauso wa binadamu, nge na simba au mvyauso wa simba, popo na nge
Mbilikimo (Ulaya) Zimwi mdogo wa ardhi
Mchawi (Duniani kote) Mtu mwenye uweza ya ajabu
Milihoi (Uswahili) Pepo mbaya
Minotauri (Ugiriki) Mtu mwenye kichwa cha fahali
Monosero (Ulaya) Mvyauso wa kulungu, farasi, tembo na nguruwe mwenye pembe moja
Mtu-fisi (Afrika) Mtu awezaye kugeuza fisi
Mtu-mbwa (Duniani wote) Mtu awezaye kugeuza mbwa
Mumiani (Uswahili) Kiumbe kama vampiri anyonyaye damu
Muza (Ugiriki) Zimwi wa fani
Mzimu (Uswahili) Pepo wa mababu
Mzuka (Duniani kote) Pepo wa marehemu
N
haririNayadi (Ugiriki) Nimfa wa maji baridi
Ndegeradi (Amerika ya Kaskazini) Pepo wa radi mwenye umbo la ndege
Nereidi (Ugiriki) Nimfa wa bahari na binti wa Nereo
Ngoloko (Uswahili) Pepo waishio katika mabwawa ya mikoko
Nguva (Duniani kote) Mvyauso wa binadamu na samaki
Nimfa (Ugiriki) Zimwi wa msitu
Nusumungu (Duniani kote) Nusu binadamu na nusu mungu
O
haririOkeanidi (Ugiriki) Nimfa wa bahari na binti wa Okeano
Onosentauri (Ulaya) Mvyauso wa binadamu na punda
Oreadi (Ugiriki) Nimfa wa milima
P
haririPandikizi la mtu (Ulaya) Madubwana wabaya wanaofanana na binadamu
Pegasi (Ugiriki) Farasi mwenye mabawa
Pepo (Duniani kote) Zimwi mtundu
Pepopunda (Uswahili) Pepo mbaya
Piksi (Uingereza) Zimwi mdogo sana
S
haririSaskwachi (Amerika ya Kaskazini) (pia: Mguumkubwa) Kiumbe mdogo kama sokwe
Satiri (Ugiriki) Mvyauso wa mbuzi na binadamu
Sentauri (Ugiriki) Mvyauso wa farasi na binadamu
Serbero (Ugiriki) Mbwa mwenye vichwa vitatu
Sfinksi (Ugiriki) Simba mwenye maziwa na kichwa cha mwanamke na mabawa
Shetani (Duniani kote) Malaika mbaya wa Biblia
Siklopsi (Ugiriki) Majitu chongo
Silfi (Ulaya) Zimwi wa hewa
Sireni (Ugiriki) Zimwi wa maji wenye kichwa cha mwanamke na mwili wa ndege
Skila (Ugiriki) Mvyauso wa mwanamke mwenye mkia wa nyoka, miguu kumi na miwili ya mbwa
Spriti (Ulaya) Zimwi kama pepo au elfi.
Sukubi (Ulaya) Shetani wa kike wa usiku abakaye wanaume katika jinamizi
T
haririThula (Ugiriki) Orka mkubwa katika mitholojia ya Kigiriki
Titani (Ugiriki) Watoto-majitu wa Urano na Gaya
Troli (Skandinavia) Pepo wa msitu
U
haririUndini (Ulaya) Zimwi wa maji
Unikorni (Ulaya) Farasi mwenye pembe moja
V
haririValkirya (Skandinavia) Zimwi wa kike ambao wamepanda farasi wenye mabawa
Vampiri (Duniani kote) Jina la Ulaya ya mumiani; Kuwa anyonyaye damu
W
haririWiverni (Uingereza) Joka wa Uingereza wenye miguu miwili na mabawa mawili
Y
haririYeti (Uhindi, Uchina, Mongolia na Nepali) Dubwana la theluji kama saskwachi