Panya-nyika
Panya-nyika | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Panya-nyika wa Mlima Kenya (Otomys orestes)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 21:
|
Panya-nyika ni wanyama wagugunaji wa jenasi Otomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika nyika nyevu mpaka nyanda za juu na vinamasi vya milimani.
Maelezo
haririPanya-nyika ni wagugunaji imara wenye uelekeo wa kuwa na uso mfupi na miguu mifupi kuliko spishi nyingine za panya. Mwili wao una urefu wa sm 12-22 na uzito wa g 90-260. Mkia pia ni mfupi kuliko panya wengi sana, kwa kawaida kati ya moja na mbili ya tatu ya urefu wa mwili. Rangi ya manyoya inatofautiana kulingana na spishi, lakini kwa ujumla huwa na manyoya kahawia hadi kijivu ambayo ni kawaida kwa panya na wagugunaji wengine wadogo wa porini, ingawa rangi ya upande wa chini ni hafifu zaidi. Spishi zinazoishi katika maeneo yenye joto kubwa au ya wastani huwa na masikio makubwa sana miongoni mwa panya, huku baadhi ya spishi za milimani zikiwa na masikio madogo zaidi. Vidole vyao vyote vina kucha ndefu na kucha za nyuma ni ndefu kuliko kucha za mbele.
Spishi nyingi sana huishi kwenye maeneo manyevu, nyika na makazi yalandanayo na hula mimea ya maeneo hayo, wakiiongezea mara kwa mara mizizi na mbegu. Hizo ni spishi za ardhini ambazo hukaa juu ya ardhi katika viota wazi vilivyo na umbo la bakuli na vilivyotengenezwa na nyasi zilizokatwa-katwa karibu na maeneo yenye mabwawa na uoto mzito.
Mwenendo
haririPanya-nyika hukiakia wakati wa alasiri na alfajiri. Wengi sana hushughulika mchana, ingawa panya-nyika wengine huonyesha shughuli za usiku. Wanaunda na kugawana njia za kukimbia na spishi nyingine zilizopo pamoja nao kupitia uoto wakati wanajilisha kwa mimea kijani.
Panya hao ni walamani thabiti na sehemu kubwa ya mchakato wa kumeng'enya hufanyika katika sikamu kwa msaada wa vijidudu. Vidonge vya kinyesi mara nyingi hunyweshwa tena ili kupata zaidi kutoka kwa chakula duni kwa virutubisho. Chakula chao kina mashina na majani ya nyasi, mimea na vichaka, na mbegu za nyasi. Walakini, sio wachaguzi wa chakula na watakula karibu spishi zote za mimea kijani katika makazi yao. Spishi fulani pia zinaweza kuguguna gome la misonobari kwenye migunda wakiharibu miti hii. Wametoholewa kuwa na kiwango cha uvumilivu wa hali ya juu kwa mimea yenye sumu.
Kwa kawaida huishi peke yao na kugombana na wana wengine wa spishi yao. Madume wapevu hutunza mara nyingi eneo dogo la kinyumba karibu na mahali pa kiota. Wanawasiliana kupitia ishara za kunusa kwa kutopoa eneo lao kwa vinyaa vya tezi za mkundu. Wakati wanyama wenye cheo sawa wanapokutana huanza kupigana na kufukuzana hadi mnyama mmoja atakapokimbia au kuonyesha tabia ya unyenyekevu. Tabia za kunyenyekea ni pamoja na kukaa wima na kufunua tumbo wakitatarika. Mapigano hayo mara nyingi husababisha majeraha, makubwa pengine.
Spishi
hariri- Otomys anchietae (Angolan vlei rat)
- Otomys angoniensis, Panya-nyika wa Angoni (Angoni vlei rat)
- Otomys barbouri, Panya-nyika wa Barbour (Barbour's vlei rat)
- Otomys burtoni (Burton's vlei rat)
- Otomys cheesmani (Cheesman's vlei rat)
- Otomys cuanzensis (Cuanza vlei rat)
- Otomys dartmouthi, Panya-nyika wa Ruwenzori (Ruwenzori vlei rat)
- Otomys denti, Panya-nyika wa Dent (Dent's vlei rat)
- Otomys dollmani, Panya-nyika wa Dollman (Dollman's vlei rat)
- Otomys fortior (Kaffa vlei rat)
- Otomys helleri (Heller's vlei rat)
- Otomys irroratus (Southern African vlei rat)
- Otomys jacksoni, Panya-nyika wa Ml. Elgon (Mount Elgon vlei rat)
- Otomys lacustris, Panya-nyika wa Tanzania (Tanzanian vlei rat)
- Otomys laminatus (Laminate vlei rat)
- Otomys maximus (Large vlei rat)
- Otomys occidentalis (Western vlei rat)
- Otomys orestes, Panya-nyika wa Ml. Kenya (Afroalpine vlei rat)
- Otomys saundersiae (Saunder's vlei rat)
- Otomys simiensis (Simien Mountains vlei rat)
- Otomys thomasi, Panya-nyika wa Mau (Thomas's vlei rat)
- Otomys tropicalis, Panya-nyika wa Aberdares (Tropical vlei rat)
- Otomys typus (Typical vlei rat)
- Otomys uzungwensis, Panya-nyika wa Udzungwe (Uzungwe vlei rat)
- Otomys yaldeni (Yalden's vlei rat)
- Otomys zinki, Panya-nyika wa Ml. Kilimanjaro (Mt. Kilimanjaro vlei rat)
Picha
hariri-
Panya-nyika wa Afrika ya Kusini