Papa Yohane Paulo I
Papa Yohane Paulo I (17 Oktoba 1912 – 28 Septemba 1978) alikuwa Papa kwa siku 33 tu kuanzia 26 Agosti/3 Septemba 1978 hadi kifo chake[1] kilichotokea ghafla usiku kutokana na ugonjwa wa moyo uliomsumbua tangu zamani.
Alitokea Forno di Casale, Belluno, Italia Kaskazini[2], jina lake la awali lilikuwa Albino Luciani.
Baada ya kuchaguliwa na makardinali wenzake, alijitajia jina linalounganisha yale ya Mapapa wawili waliomtangulia (Papa Yohane XXIII, halafu Papa Paulo VI) ili kuonyesha nia yake ya kuendeleza kazi yao, hasa Mtaguso wa pili wa Vatikano. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Papa kuchagua jina dabo.
Ingawa muda haukumruhusu kutekeleza mipango yake, aliacha kumbukumbu nzuri ya wema wake (aliitwa "Papa wa tabasamu").
Aliyechaguliwa badala yake alijiwekea lengo hilohilo akajiita Papa Yohane Paulo II.
Ametangazwa Mwenye heri tarehe 4 Septemba 2022.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Agosti.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Yohane Paulo I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |