Patrick wa Ireland

Patrick wa Ireland (kwa Kilatini Patricius) aliishi kuanzia mwaka 387 hivi hadi tarehe 17 Machi 461[1] (wengine wanasema 493[2]).

Mt. Patrick katika kioo cha rangi.
Mahali panapodhaniwa kuwa alifanyiwa mazishi huko Downpatrick.

Ni maarufu kama Mkristo kutoka Uingereza aliyepata kuwa mmisionari mkuu wa Ireland na anaheshimiwa kama mtakatifu msimamizi wa kisiwa hicho.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Maisha

hariri

Kati ya maandishi yake, zimetufikia barua mbili, ambamo tunapata habari za kuaminika juu yake, tofauti na nyingine nyingi ambazo zinatia shaka.[4]

Alipokuwa na umri wa miaka 16 hivi huko Wales, alitekwa na maharamia kutoka Ireland na kufanywa mtumwa kisiwani huko.

Baada ya miaka 6 alifaulu kukimbia na kurudi kwenye familia yake.

Lakini akajisikia wito wa kuinjilisha wakazi wa kisiwa hicho, hivyo baada ya kujiandaa katika monasteri ya Ufaransa akarudi huko kama askofu akafanya kazi hasa kaskazini na magharibi akitangaza kwa bidii Injili kwa wote na kuongoza kwa nguvu Kanisa lake.[5]

Sala yake

hariri

Kristo uwe nami, Kristo uwe ndani mwangu,

Kristo nyuma yangu, Kristo mbele yangu,

Kristo karibu nami, Kristo ili unitawale,

Kristo, ili unifariji na kunifundisha,

Kristo pamoja nami, Kristo juu yangu,

Kristo katika amani, Kristo katika hatari,

Kristo moyoni mwa wote wanaonipenda,

Kristo mdomoni mwa rafiki na mgeni.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Common Worship: Services and Prayers for the Church of England, The Calendar, p. 7
  2. St Patrick in the Catholic Encyclopedia (1913).
  3. Martyrologium Romanum
  4. Macthéni, Muirchú maccu; White, Newport John Davis (1920). St. Patrick, his writings and life. New York: The Macmillan Company. ku. 31–51, 54–60.
  5. All About Saint Patrick's Day Church Year Retrieved 2011-02-20

Marejeo

hariri
  • Brown, Peter (2003), The rise of Western Christendom : triumph and diversity, A.D. 200-1000 (tol. la 2nd), Oxford: Blackwell, ISBN 0-631-22138-7
  • Bury, John Bagnell (1905), Life of St. Patrick and his Place in History, London{{citation}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
  • Byrne, Francis J. (1973), Irish Kings and High-Kings., London: Batsford, ISBN 0-7134-5882-8
  • Cahill, Thomas (1995), How the Irish Saved Civilization, New York: Doubleday, ISBN 0-385-41849-3
  • Charles-Edwards, T. M. (2000), Early Christian Ireland, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 0-521-36395-0
  • Dark, Ken (2000), Britain and the end of the Roman Empire, Stroud: Tempus, ISBN 0-7524-2532-3
  • De Paor, Liam (1993), Saint Patrick's World: The Christian Culture of Ireland's Apostolic Age, Dublin: Four Courts Press, ISBN 1-85182-144-9
  • Duffy, Seán,, mhr. (1997), Atlas of Irish History, Dublin: Gill and Macmillan, ISBN 0-7171-3093-2{{citation}}: CS1 maint: extra punctuation (link) CS1 maint: multiple names: editors list (link)
  • Dumville, David (1994), "The Death date of St. Patrick"", katika Howlett, David (mhr.), The Book of Letters of Saint Patrick the Bishop., Dublin: Four Courts Press, ISBN 1-85182-136-8
  • Fletcher, Richard (1997), The Conversion of Europe: From Paganism to Christianity 371–1386 AD., London: Harper Collins, ISBN 0-00-686302-7
  • Hood, A. B. E (1978), St. Patrick: his Writings, and Muirchú's Life, London and Chichester: Phillimore, ISBN 0-85033-299-0
  • Hughes, Kathleen (1972), Early Christian Ireland: Introduction to the Sources, London: Hodder & Stoughton, ISBN 0-340-16145-0
  • Iannello, Fausto (2008), "Note storiche sull'Epistola ad Milites Corotici di San Patrizio", Atti della Accademia Peloritana dei Pericolanti, classe di Lettere, Filosofia e Belle Arti, 84: 275–285
  •   Moran, Patrick Francis Cardinal (1913). "St. Patrick". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
  • McCaffrey, Carmel (2003), In Search of Ancient Ireland, Chicago: Ivan R Dee, ISBN 978-1-56663-525-7
  • MacQuarrie, Alan (1997), The Saints of Scotland: Essays in Scottish Church History AD 450–1093, Edinburgh: John Donald, ISBN 0-85976-446-X
  • Ó Cróinín, Dáibhí (1995), Early Medieval Ireland: 400–1200, London: Longman, ISBN 0-582-01565-0
  • O'Loughlin, Thomas (1999), Saint Patrick: The Man and his Works, London: S.P.C.K.
  • O'Loughlin, Thomas (2000), Celtic Theology, London: Continuum
  • O'Loughlin, Thomas (2005), Discovering Saint Patrick, New York: Orbis
  • O'Loughlin, Thomas (2005), Analecta Bollandiana, 123: 79–89 {{citation}}: |contribution= ignored (help); Missing or empty |title= (help)
  • O'Loughlin, Thomas (2007), Nagy, J. F. (mhr.), The myth of Insularity and nationality in Ireland, Dublin: Four Courts Press, ku. 132–140
  • O'Rahilly, T. F. (1942), The Two Patricks: A Lecture on the History of Christianity in Fifth-Century Ireland, Dublin: Dublin Institute for Advanced Studies
  • Stancliffe, Claire (2004). "Patrick (fl. 5th cent.)". Oxford Dictionary of National Biography. Oxford University Press. Iliwekwa mnamo 2007-02-17. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameters: |month= na |coauthors= (help)
  • Thomas, Charles (1981), Christianity in Roman Britain to AD 500, London: Batsford, ISBN 0-7134-1442-1
  • Wood, Ian (2001), The Missionary Life: Saints and the Evangelisation of Europe 400-1050, London: Longman, ISBN 0-582-31213-2
  • Yorke, Barbara (2006), The Conversion of Britain: Religion, Politics and Society in Britain c.600–800, London: Longman, ISBN 0-582-77292-3

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.