Petrider Paul
Petrider Paul ni mwanamke Mtanzania aliye mtetezi wa haki za wasichana na wanawake kwa ujumla.[1]. Ni mwanzilishi mwenza wa shirika la Youth for Change Tanzania (kwa kiswahili - Vijana Kwa Mabadiliko Tanzania[2].
Petrider Paul | |
Petrider Paul | |
Amezaliwa | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | Mtetezi wa haki za wasichana na wanawake |
Tarehe 31 Oktoba 2018, akiwa na umri wa miaka 24, Kamishna ya Umoja wa Afrika ilimteua kuwa mwanachama wa Bodi ya Ushauri ya Vijana wa Afrika katika masuala ya maendeleo ya vijana[3].
Harakati tangu miaka 15
haririPetrider akiwa na umri wa miaka 15 alianza kufanya kazi zake za harakati za kumtetea msichana dhidi ya ukatili pale alipotambua kwamba haki za watoto wengi hasa wasichana zinakiukwa katika jamii yake.[4]. Alikuwa miongoni mwa wanachama wa kwanza katika jopo la ushauri la vijana la Idara ya Serikali ya Uingereza.[5]
Shauku katika Elimu
haririPetrider Paul ana shauku katika elimu na anaamini kuwa wasichana hawathaminiki au wanapewa thamani ya chini tangu kuzaliwa kwao, mila katika nchi mara nyingi zikiwa zinachangia katika hilo. Hajawahi kupendezwa kuona msichana akitendwa vibaya. [6]
Wasifu Kielimu
haririPetrider Paul ana Stashahada ya Uzamili katika Uchumi wa Diplomasia kutoka katika Chuo cha Diplomasia kilichopo Tanzania. Pia ana Shahada ya Sanaa katika Mahusiano ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma. [7].
Kazi
haririAnafanya kazi na Umoja wa Afrika kama mwanachama katika bodi ya Ushauri ya Vijana wa Afrika katika masuala ya maendeleo ya vijana. Pia ni mwakilishi wa Tanzania katika bunge la vijana [8]
Mikutano ya Kimataifa aliyohudhuria
haririThe Afican Girls' Summit ( Mkutano wa Wasichana wa Kiafrika) - wa kupinga ndoa za utotoni, The One Young World Summit ( Mkutano wa Mmoja Mchanga Duniani), na The Girls Not Brides global meeting ( Mkutano wa dunia wa Wasichana sio Wanamwali) - wa kupinga ndoa za utotoni.[9].
Tuzo
haririQueen's Young Leaders Award - 2016.[10]
Viungo vya Nje
hariri- Petrider Paul - YouTube Channel
- Petrider Paul Ilihifadhiwa 1 Novemba 2020 kwenye Wayback Machine. Tovuti rasmi
Tanbihi
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-08.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-20. Iliwekwa mnamo 2020-04-08.
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/Tanzanian-woman-gets-key-role-in-AU-Youth-Board/1840340-4856994-s3m95m/index.html