Petro Baptista
Petro Baptista (kwa Kihispania San Pedro Bautista), alikuwa balozi wa Hispania nchini Japani, mkuu wa Ndugu Wadogo Pekupeku wamisionari huko, padri aliyehudumia wakoma, na hatimaye akawa kiongozi wa wafiadini 26 waliouawa msalabani tarehe 5 Februari 1597.
Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 14 Septemba 1627, halafu Papa Pius IX akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Juni 1862.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[1].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |