Petro wa Verona, O.P. (Verona, Veneto, 1206Lombardia, 6 Aprili 1252) alikuwa padri wa Italia Kaskazini na mmojawapo kati ya Wadominiko waliofia dini nchini mwake.

Mchoro wa Pedro Berruguete ukimwonyesha Mt. Petro mfiadini.

Wazazi wake walikuwa wafuasi wa Mani, lakini mwenyewe utotoni alijiunga na Kanisa Katoliki halafu ujanani Dominiko Guzman alimpokea katika shirika lake jipya.

Alijitosa kupambana na uzushi kwa kila njia.

Kama alivyotamani na kuomba, aliuawa na mzushi akiwa njiani kati ya Milano na Como. Kufani alikuwa akikiri imani sahihi[1]. Baadaye muuaji wake, Karino wa Balsamo, alitubu na kujiunga na utawa kama bruda, naye anaheshimiwa kama mwenye heri.

Petro anaheshimiwa kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Inosenti IV tarehe 9 Machi 1253, upesi kuliko mwingine yeyote[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Aprili[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/51250
  2. Donald Prudlo, The martyred inquisitor: the life and cult of Peter of Verona (Aldershot: Ashgate Publishing, 2008), p. 81, esp. note 35.
  3. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Marejeo hariri

  • Dondaine, Fr. Antoine, O.P. "Saint Pierre Martyr" Archivum Fratrum Praedicatorum 23 (1953): 66-162.
  • Prudlo, Donald. The Martyred Inquisitor: The Life and Cult of Peter of Verona (+1252). Aldershot: Ashgate Press, 2008.
  • Prudlo, Donald. "The Assassin-Saint: The Life and Cult of Carino of Balsamo", Catholic Historical Review, 94 (2008): 1-21.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.