Rehoboamu
Rehoboamu (kwa Kiebrania: רְחַבְעָם, Rəẖavʻam au Reḥaḇʻām; kwa Kigiriki: Ροβοαμ, Rovoam; kwa Kilatini: Roboam; 970 KK-910 KK hivi) alikuwa mfalme wa nne wa Israeli.
Habari zake zinapatikana katika Biblia (Kitabu cha Kwanza cha Wafalme na kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati).
Alikuwa mtoto na mrithi wa Solomoni[1], lakini alisababisha uasi wa makabila ya kaskazini yakiongozwa na Yeroboamu I, akajikuta amebaki na yale ya kusini tu.
Kadiri ya Kitabu cha Kwanza cha Wafalme (12:22-24) na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati (11:2-4; 12:5-7) nabii Shemaya alimzuia Rehoboamu asipigane vita na Yeroboamu I ili kujirudishia mamlaka juu ya makabila hayo yaliyoasi[2].
Pia alimtabiria adhabu ya Mungu kumpitia farao Shishak wa Misri kwa makosa yake.
Mama wa Rehoboamu alikuwa si Mwisraeli, bali Mwamoni. Mwenyewe alioa wake 18 na masuria 60 na kupata watoto 88: 28 wa kiume na 60 wa kike.
Rehoboamu alitawala miaka 17 akarithiwa na mwanae Abiya.
Tanbihi
hariri- ↑ "Before the death of Solomon the apparently unified kingdom of David began to disintegrate. With Damascus independent and a powerful man of Ephraim, the most prominent of the Ten Tribes, awaiting his opportunity, the future of Solomon's kingdom became dubious". Rehoboam". Jewish Encyclopedia. 1906.
- ↑ Pulpit Commentary on 1 Kings 12, accessed 17 October 2017
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rehoboamu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |