Roderiko Aguilar
(Elekezwa kutoka Rodrigo Aguilar Alemán)
Roderiko Aguilar (kwa Kihispania Rodrigo Aguilar Alemán, Sayula, 13 Mei 1875 - Ejutla, Jalisco, Mexico, 28 Oktoba 1927) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Meksiko hadi alipouawa bila kesi kwa kutundikwa na askari mtini wakati wa Vita vya Wakristero. Hivyo alijaliwa kufia dini yake kama alivyotamani sana [1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Novemba 1992 halafu mtakatifu mfiadini tarehe 21 Mei 2000 pamoja na wenzake 24 waliofia dini katika vita hivyo[2]:
Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 21 Mei ila ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90113
- ↑ "List of San Cristobal and companions, St. Cristobal Magallanes and Companions Church, Mission, Texas". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-24. Iliwekwa mnamo 2020-10-27.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |