Roeperocharis bennettiana
Roeperocharis bennettiana | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Roeperocharis bennettiana ni spishi ya okidi ya nchi kavu yenye asili ya Afrika Mashariki. Ni moja ya spishi 4 za jenasi Roeperocharis ambazo zinajulikana hadi mwaka 2014. [1] Aina hii ya okidi imeripotiwa kukua kwenye uoto wa misitu, mbuga na nyanda za nyasi.
Muundo
haririMimea ya spishi hii hukua kutoka kwa mzizi-kiazi yenye umbo la duara kutoka chini ya ardhi na kufikia urefu wa hadi sm 95. Majani yake yana urefu wa sentimita 25 na upana wa sentimita 2.5. Mimea hutoa maua ya manjano inayoelekea kijani au kijani kabisa. [2]
Maua ya R. bennettiana huchanua mwezi Februari katika Nyanda za Juu za Kusini Tanzania. [2] Pia, mmea huu umeripotiwa kukua kwenye Mlima Namuli nchini Msumbiji. [3] [4]
Angalia pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Cribb, Phillip; Leedal, G. Phillip (1982). The Mountain Flowers of Southern Tanzania.
- ↑ 2.0 2.1 Cribb, Phillip; Leedal, G. Phillip (1982). The Mountain Flowers of Southern Tanzania.Cribb, Phillip; Leedal, G. Phillip (1982). The Mountain Flowers of Southern Tanzania.
- ↑ https://www.mozambiqueflora.com/speciesdata/species.php?species_id=209310
- ↑ Harris, T.; Darbyshire, I.; Polhill, R (Julai 2011). "New species and range extensions from Mt Namuli, Mt Mabu and Mt Chiperone in northern Mozambique". Kew Bulletin. 66. doi:10.1007/s12225-011-9277-9.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Roeperocharis bennettiana kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |