Rogeli na Abdalah (walifariki Cordoba, Hispania, 852) walikuwa Wakristo kutoka Syria waliouawa kwa kukatwa mikono, miguu na hatimaye kichwa na Waislamu waliotawala nchi hiyo[1].

Rojelo alikuwa mmonaki mzee, Abdalah alikuwa kijana. Waliingia mskitini na kuanza kuhubiri Injili.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Septemba[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.