'

Saed Kubenea
Majina mengineMchanja mbuga
Kazi yakeMwandishi wa habari


Saed Kubenea alikuwa mbunge wa jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kupitia chama cha CHADEMA hadi uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Jimbo la Ubungo ni moja ya majimbo yaliyomo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo kambi ya upinzani ilifanikiwa kuyatwaa kupitia uchaguzi huo wa mwaka 2015 na kuwezesha kubeba viti vingi vya udiwani na hatimaye kushinda viti vya umeya. Upinzani ulitwaa kiti cha umeya cha Manispaa ya Kinondoni na baadaye Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Baadaye Wilaya ya Kinondoni iligawanywa na kuzaliwa manispaa ya Ubungo ikafanya uchaguzi mpya wa meya. Kinondoni ikachukuliwa na CCM katika uchaguzi uliojaa visa na upinzani kupitia mgombea wa Chadema, Boniface Jacob, ikatwaa kiti cha Ubungo.

Kabenea anaendelea kuwa mmiliki na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kitanzania Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inayochapisha magazeti ya MwanaHALISI, MwanaHALISI Online, MwanaHALISI Forum na MSETO.[1] lakini magazeti hayo yalifunguliwa tu tarehe 10 Februari 2022 [2].

Gazeti la MwanaHALISI lililozaliwa Mei 2006 lilianza kupata msukosuko na serikali mwaka 2008 lilipofungiwa kwa mara ya kwanza kwa siku 90 (miezi mitatu). Mara ya pili likaja kufungiwa Juni 2012 kwa kuandika habari ya kiuchunguzi iliyobainisha mtandao uliopanga na kutekeleza njama ya kumteka na kumtesa karibu ya kumuua, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka wakati huo kikiwa kimetangaza mgogoro wa kimaslahi na Serikali. Mara ya tatu MwanaHALISI likafungiwa na serikali Septemba 2017. Wakati adhabu ya miezi mitatu ilimalizika, adhabu zilizofuatia zilifutwa na Mahakama Kuu baada kukubali pingamizi zilizofunguliwa na HHPL. Hata hivyo, mara ya mwisho serikali imeendelea kuzuia kuchapishwa tena kwa gazeti hilo kwa kutotoa leseni.

Anafahamika sana kwa kutoa habari nyingi za msingi wa makatazo na machukio dhidi ya watu walio mafisadi katika serikali ya watu wa Tanzania. Ni mwandishi mwenye malumbano makubwa kabisa katika nchi ya Tanzania.

Tarehe 5 Januari 2008 alivamiwa ofisini mwake na kumwagiwa tindikali na watu wasiofahamika (saedkubenea.blogsport.com) ikambidi apelekwe nchini India kwa matibabu.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Hata hivyo Gazeti la Mseto lilifungiwa na Serikali tarehe 11 Agosti 2016 kwa kipindi cha miezi 36 (miaka mitatu) kwa madai ya kuchapisha habari iliyoambatana na nyaraka za kughushi
  2. https://www.yahoo.com/news/tanzania-lifts-ban-four-newspapers-143341774.html

Viungo vya nje hariri