Sarafina!
Sarafina! ni mchezo wa kuigiza wa kimuziki kutoka Afrika ya Kusini iliyotungwa na Mbongeni Ngema inayoonyesha wanafunzi wakishiriki katika maandamano ya Soweto wakipinga ubaguzi wa rangi.
Sarafina! | |
---|---|
Imeongozwa na | Darrell Roodt |
Imetungwa na | Mbongeni Ngema William Nicholson |
Nyota | Leleti Khumalo Whoopi Goldberg Miriam Makeba John Kani |
Muziki na | Mbongeni Ngema Stanley Myers Hugh Masekela |
Imehaririwa na | David Heitner |
Imesambazwa na | Buena Vista Pictures (USA) Warner Bros. (International) |
Imetolewa tar. | 18 Septemba, 1992 |
Ina muda wa dk. | 117 minutes |
Nchi | South Africa France United Kingdom United States |
Lugha | English |
Ilitengenezwa pia kama filamu mwaka 1992 ikichezwa na Leleti Khumalo, Whoopi Goldberg, Miriam Makeba, John Kani na Tertius Meintjies.
Hatua ya uzalishaji
haririSarafina! ilionyeshwa awali Broadway tarehe 28 Januari 1988, katika Cort Theatre, na ilifungwa tarehe 2 Julai 1989, baada ya maonyesho 597 na vidokezo 11. Sarafina ilibuniwa na kuongozwa na Mbongeni Ngema ambaye aliandika pia kitabu muziki, na nyimbo. Ilionyeshwa mara ya kwanza katika The Market Theatre, Johannesburg, Afrika ya Kusini, mwezi Juni 1987. Msanii Leleti Khumalo alicheza kama Sarafina.
Leleti Khumalo ametunikiwa Tony Award, Mwigizaji bora katika mchezo wa kuigiza wa kimuziki, vilevile tuzo la NAACP kwa ajili ya ustadi wake. Uzalishaji wenyewe pia ulishinda tuzo la Tony Award kwa: Muziki bora, Densi bora, na Mwelekeo wa Juu Zaidi.
Filamu
haririFilamu ilitolewa tarehe 18 Septemba 1992. Filamu ilifanywa Soweto na Johannesburg, Afrika ya Kusini. Darrell Roodt aliiongoza, kutumia maudhui ya Mbongeni Ngema na William Nicholson. Leleti Khumalo bado alicheza kama Sarafina, pamoja na Whoopi Goldberg kama Maria Masombuka na Miriam Makeba kama Angelina.
Makampuni yaliyohusika yalikuwa miongoni mwa British Broadcasting Corporation (BBC). Katika Umoja wa Mataifa, shirika la filamu la MPAA, liliweka kanuni ya PG-13 kwa maonyesho ya vurugu inayosababishwa na ubaguzi wa rangi. Filamu iliyoongezwa, iliyotolewa mwaka 1993, ilipata kiwango cha R kwa maonyesho ya ghasia ghasia.
Kwa Whoopi Goldberg, hii ilikuwa mradi alikuwa amedhamiria kuchangia, na aliwashawishi watendaji katika Disney kwamba kama wangekubaliana kufanya hii filamu, angeweza kukubali kuigiza kama Dolores Van Cartier katika [2] ambayo Disney ilikuwa ina nia ya kuifanya tangu mananke awali ilileta mamilioni nyingi duniani kote.
Filamu ilitolewa katika mashindano ya Cannes Film Festival 1992. [1]
Vitimbi
haririHadithi yenyewe inahusu wanafunzi walioshiriki katika maandamano Soweto, wakipinga utekelezaji wa Kiafrikaans kama lugha ya kufundisha katika shule. Inatoa toleo linachomoza shule sawa na maandamano ya Soweto tarehe 16 Juni 1976. Msimuliaji hutujulisha kuhusu watu kadhaa miongoni mwao msichana wa shule mwanaharakati aitwaye Sarafina. Maji huzidi unga wakati polisi wanapowapiga risasi wanafunzi kadhaa darasani. Hata hivyo, mwisho ya onyesho hili huwa ni la furaha na kwaheri za wanafunzi wanaotoka shule, ambayo inachukua sehemu ya pili ya filamu.
Katika toleo la filamu Sarafina anahisi aibu wakati mamake (amechezwa na Miriam Makeba katika filamu) alikubali wajibu wake kama mtumishi wa ndani katika nyumba ya Wazungu katika ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini, na aliwahamasisha wenzake kusimama katika maandamano, hasa baada ya mwalimu wake, Maria Masombuka (amechezwa na Whoopi Goldberg katika filamu) kufungwa.
Sehemu ya Mkurugenzi
haririSarafina! ilionyeshwa katika Afrika ya Kusini tarehe 16 Juni 2006 ili kuadhimisha miaka 30 baada ya maandamano ya Soweto.
Sehemu ya Mkurugenzi haijatofautiana sana na ya awali, isipokuwa kuongezwa kwa kipande ambacho hakikuwemo katika toleo la asili, kati ya Leleti Khumalo (Sarafina) na Miriam Makeba (mamake Sarafina), ambayo imeongezwa na wimbo Thank You Mama.
Marejeo
hariri- ↑ "Festival de Cannes: Sarafina". festival-cannes.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-05. Iliwekwa mnamo 2009-08-17.