Miriam Makeba
Miriam Makeba (4 Machi 1932 – 10 Novemba 2008), aliyeitwa pia Mama Afrika, alikuwa mwanamuziki kutoka nchi ya Afrika Kusini. Yeye ni mashuhuri hasa kwa kufahamisha muziki wa Afrika nje ya bara lake.
Miriam Makeba | |
Amezaliwa | 4 machi 1932 Johannesburg |
---|---|
Amekufa | 10 November 2008 Italia |
Nchi | Afrika Kusini |
Majina mengine | Miriam Makeba |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Maisha
haririMiriam Makeba alizaliwa tarehe 4 Machi 1932 katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini. Mama yake alikuwa wa kabila la waswazi|Swazi sangoma na baba yake wa kabila la Xhosa. Baba alifariki wakati Miriam akiwa na umri wa miaka sita.
Miriam alikuwa mwanamuziki pekee wakati huo aliyeweza kufanikiwa kuzieneza nyimbo zenye asili ya Kiafrika. Pia alikuwa miongoni mwa wanamuziki waasisi wa kuchanganya mitindo tofauti ya muziki na kutengeneza muziki wa kuvutia kama kwaito.
Alianza kazi ya muziki mwanzoni mwa mwaka 1950 akiwa na kundi la The Skylarks, baadaye alijiunga na kundi la Manhattan Brothers. Makundi hayo yalikuwa yakipiga muziki wa Jazz wenye vionjo vya Kiafrika kusini.
Mwaka 1959, Miriam alifanya onyesho kubwa pamoja na Hugh Masekela, mume wake wa baadaye. Maonyesho aliyofanya pamoja na albamu nzuri alizorekodi havikumpatia faida, lakini baadaye alifanya matamasha katika nchi za Ulaya na Amerika.
Ulipoanza mkakati wa kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendelea Afrika ya kusini, Miriam aliamua kurudi nyumbani kupigania uhuru. Baadaye alialikwa Italia katika tamasha la filamu la Venice.
Kati ya nyimbo za Miriam zilizo maarufu ni Patapata (kwa lugha ya KiXhosa ni "Qongaqothwan"). Wimbo maarufu wa Malaika uliotungwa na Fadhili William Miriam aliuimba akishirikiana na Harry Belafonte.
Miriam alirudi tena nyumbani mwaka 1990, na mwaka 1992 alicheza filamu ya Sarafina.
Mwaka 2001 alitunukiwa tuzo ya dhahabu iliyoitwa Otto Hahn Peace Medal, pia alishika nafasi ya 38 kati ya wanamuziki bora kati ya 100 waliopewa tuzo nchini Afrika Kusini.
Mwaka wa 2005, Miriam alifanya ziara ya kimuziki kwa ajili ya kuwaaga marafiki wake wote duniani iliyomchukua miezi kumi na minne; alifanya maonyesho katika nchi zote alizotembelea wakati alipokuwa akifanya kazi ya muziki.
Aliaga dunia kwa shtuko la moyo alfajiri ya tarehe 10 Novemba 2008, nchini Italia baada ya kutoa onyesho la muziki.
Orodha ya Albamu Kadhaa
hariri- Something New from Africa (1959)
- New Sounds of Africa (1959)
- The Many Voices of Miriam Makeba (1960)
- Miriam Makeba (album)|Miriam Makeba (1960)
- The World of Miriam Makeba (1963)
- The Voice of Africa (1964)
- Makeba Sings (1965)
- An Evening with Belafonte/Makeba (1965)
- The Magic of Makeba (1966)
- The Magnificent Miriam Makeba (1966)
- Miriam Makeba in Concert (1967)
- All About Miriam (1967)
- Pata Pata (1967)
- Makeba! (1968)
- Live in Tokyo (1968)
- The Best of Miriam Makeba (1968)
- Keep Me in Mind (1970)
- Forbidden Games (1973)
- A Promise (1974)
- Live in Conakry (pia Appel a l'Afrique, 1974)
- Miriam Makeba & Bongi (1975)
- Live in Paris (1977)
- Country Girl (pia Meet Me at the River, 1978)
- Comme une symphonie d'amour (1979)
- Sangoma (1988)
- Welela (1989)
- Kilimanjaro - Live in Conakry (pia Live au Palais du Peuple de Conakry, 1990)
- Eyes on Tomorrow (1991)
- The Queen of African Music (1991)
- Miriam Makeba and the Skylarks vol. 1 (1991)
- Miriam Makeba and the Skylarks vol. 2 (1991)
- Africa (album)|Africa (1991)
- Sing Me a Song (1993)
- Folk Songs from Africa (1994)
- Live in Paris and Conakry (1996)
- Hits and Highlights (1997)
- Homeland (2000)
- Legend (2001)
- The Guinea Years (2001)
- Mama Africa: The Very Best of Miriam Makeba (2001)
- The Definitive Collection (2002)
- The Early Years (2002)
- Reflections (2003)
- The Best of Miriam Makeba & The Skylarks (2003)
- Live at Berns Salonger, Stockholm, Sweden, 1966 (2003)
- Forever (2006)
- Her Essential Recordings (2006)
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Miriam Makeba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |