Bunilizi ya kisayansi
Bunilizi ya kisayansi (kwa Kiingereza: science fiction, inayofupishwa kama sci-fi au SF) ni aina ya fasihi, filamu, michezo ya video au sanaa. Hutumia habari za sayansi na teknolojia kuwaza hali ya wakati ujao, usafiri katika anga, usafiri wa wakati, roboti na mengineyo.
Hadithi zake zinasimuliwa mara nyingi katika ulimwengu ambao ni tofauti na ya kwetu siku hizi. Mtungaji wake atawaza mara nyingi vifaa na sayansi ambayo haipatikani leo au hata haiwezekani. Mara nyingi hadithi zake huwaziwa kutokea katika sayari tofauti pamoja na kutokea kwa viumbe visivyo wa Dunia hii.
Katika tamaduni mbalimbali kulikuwa na waandishi waliowaza safari za kwenda mahali kama mwezini na Zuhura, kwa mfano Lucianus wa Samosata[1] katika enzi ya Roma ya Kale. Lakini hali halisi fasihi hiyo ilianza tangu kupatikana kwa teknolojia ya kisasa na kutokea kwa mabadiliko ya haraka yaliyoshawishi waandishi kuwaza matumizi yake nje ya maarifa ya kawaida.
Kati ya waandishi wa kwanza wanaohesabiwa katika fani hiyo ni Mfaransa Jules Verne aliyewaza matumizi ya bunduki kubwa ili kurusha watu mwezini au H.G. Wells aliyewaza mashine ya kupeleka watu katika wakati tofauti, lakini aliwaza pia kupatikana kwa usafiri wa ndege, mashine za vita kama kifaru, runinga na vingine ambavyo vilikuwa havijagunduliwa wakati alipoandika.
Kati ya waandishi mashuhuri ni Isaac Asimov, profesa wa biokemia aliyetunga hadithi fupi nyingi za bunilizi ya kisanyasi akikumbukwa hasa kwa masimulizi yake kuhusu maadili ya roboti inayoweza kujitawala zinazoangaliwa hadi leo.
Waandishi mara nyingi hutumia SF kuelezea changamoto za siku zetu kwa kuzisimulia katika wakati ujao au sayari nyingine. Kwa njia hiyo wanalenga wasomaji watafakari mawazo yenye maana.
Marejeo
hariri- ↑ A True Story, tafsiri ya Kiingereza ya hadithi yake
Angalia mengine kuhusu Bunilizi ya kisayansi kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
- Science Fiction (Bookshelf) Ilihifadhiwa 17 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine. at Project Gutenberg
- SF Hub—resources for science fiction research, created by the University of Liverpool Library
- Science fiction fanzines (current and historical) online
- SFWA "Suggested Reading" list
- Science Fiction Museum & Hall of Fame
- Science Fiction Research Association
- A selection of articles written by Mike Ashley, Iain Sinclair and others, exploring 19th-century visions of the future. Ilihifadhiwa 18 Juni 2023 kwenye Wayback Machine. from the British Library's Discovering Literature website.
- Merril Collection of Science Fiction, Speculation and Fantasy at Toronto Public Library
- Science Fiction Studies' Chronological Bibliography of Science Fiction History, Theory, and Criticism
Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bunilizi ya kisayansi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |