Simproniani na wenzake
Simproniani na wenzake Klaudio, Nikostrati, Kastori na Simplisi (walifariki kwenye mto Sava, Panonia, leo nchini Kroasya, 306 hivi) walikuwa wachongamawe (isipokuwa Simplisi) waliouawa kwa kutupwa mtoni katika dhuluma ya Dola la Roma kwa sababu, kwa jina la Yesu Kristo, walikataa kuchonga sanamu ya mungu Eskulapi[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini. Huko Roma, kwenye Mlima Celio, walijengewa mapema basilika maarufu kwa jina la Quattro Coronati (yaani Wanne Waliotiwa Taji).
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- The Four Crowned Martyrs
- November 8, the Four Crowned Martyrs, with images of them and of Santi Quattro Coronati and the Chapel of Pope St Sylvester I
- Four Crowned Saints (or Four Crowned Martyrs) and relief at base of tabernacle, Orsanmichele
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |