Sokrates

(Elekezwa kutoka Socrates)

Sokrates (kwa Kigiriki Σωκράτης, Sōkrátēs, 470 KK399 KK) alikuwa mwanafalsafa Mgiriki (mtu wa Athens). [1]

Sokrates
Sokrates (sanamu ya kiroma katika Louvre ya Paris)
Sokrates (sanamu ya kiroma katika Louvre ya Paris)
Alizaliwa mnamo 470 KK
Alikufa mnamo 399 KK
Nchi Athens (Ugiriki ya Kale)
Kazi yake Mwanafalsafa, mwalimu

Nje ya falsafa, anajulikana hasa kwa kifo chake. Alifariki kutokana na kunywa sumu baada iliyokuwa adhabu yake kwa kupatikana na hatia katika mahakama ya watu wa Athens. Ilidaiwa kwamba mafunzo yake yaliingilia dini ya mji wa Athens na kupotosha vijana wake. Ingawa alipewa nafasi kutoroka ili kuepukana na hukumu yake na kwenda uhamishoni, Sokrates alichagua kunywa sumu hiyo kwa sababu alikuwa amekubali kwa hiari yake afuate sheria za Athens, akaamini kwamba angalikwepa hukumu yake angaliuaibisha mkataba huo.

Maarifa mengi kuhusu Sokrates yametokea katika majadiliano yaliyoandikwa na Plato, mwanafunzi wake na mwanafalsafa, maandiko ya Zenephon, mtu wa rika lake, Aristofanes, na Aristotle. Kuna matatizo katika maandiko yanayomhusu Sokrates, hivyo si vyema kutegemea chanzo kimoja tu. Ukitazama mambo yanayofanana baina ya maandiko, ukaachilia mbali mambo yanayofikiriwa kuongezwa na mwandishi, Sokrates mwenyewe ataonekana.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Anthony Gottlieb alimwita shahidi na mtakatifu wa falsafa (Monk & Raphael, 2000)
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sokrates kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.