Son Heung-min

Mchezaji wa mpira kutoka nchini Korea Kusini

Son Heung-min (alizaliwa 8 Julai 1992) ni mchezaji wa soka wa Korea Kusini ambaye anacheza kama winga au mshambuliaji wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Tottenham Hotspur na nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini.

Son akiwa Tottenham Hotspurs.

Son alizaliwa huko Chuncheon, Korea Kusini. Alianza kazi yake katika akademi ya FC Seoul, Mnamo Agosti 2008, Son alitoka kwenye akademi ya FC Seoul na kujiunga na klabu ya Hamburger ya Ujerumani.

Tarehe 13 Juni 2013, Bayer Leverkusen ilithibitisha uhamisho wa Son kwa ada ya milioni 10, ambayo ilikuwa ada kubwa zaidi ya uhamisho katika historia ya klabu wakati huo. Alikubaliana na klabu hiyo kwa muda wa miaka mitano.

Tarehe 28 Agosti 2015, Son alijiunga na klabu ya Tottenham Hotspur kwa £ milioni 22 kwa mkataba wa miaka mitano. Baada ya kusainiwa kwake, akawa mchezaji wa gharama kubwa zaidi wa Asia katika historia ya soka.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Son Heung-min kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.