Songea (mji)

Songea ni manisipaa nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma yenye postikodi namba 57100 .[1]. Eneo la mji ni wilaya ya Songea Mjini. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 131,336 [2].

Soko katika Mji wa Songea
Songea

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Tanzania" does not exist.Mahali pa mji wa Songea katika Tanzania

Majiranukta: 10°40′48″S 35°39′0″E / 10.68°S 35.65°E / -10.68; 35.65
Nchi Tanzania
Mkoa Ruvuma
Wilaya Songea Mjini
Idadi ya wakazi
 - 126,449

Kuna barabara ya lami kutoka Songea kupitia Njombe hadi barabara kuu ya Dar es Salaam - Mbeya. Barabara ya kwenda pwani kupitia Tunduru na Masasi ni mbaya mara nyingi haipitiki wakati wa mvua.

JiografiaEdit

Mji uko kwenye kimo cha m 1210 juu ya UB katika nchi ya Ungoni kwenye nyanda za juu za kusini za Tanzania. Chanzo cha mto Ruvuma kipo karibu na mji.

HistoriaEdit

Jina la Songea ni kumbukumbu ya chifu Songea wa Wangoni aliyekuwa na ikulu yake hapa wakati wa kuenea kwa ukoloni wa Ujerumani akauawa na Wajerumani wa kati wa vita ya majimaji.

Mji wa Songea (iliyoandikwa Ssongea wakati ule) ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha Kijerumani. Ukakua kuwa makao makuu ya utawala wa mkoa Songea wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Mazingira ya mji yaliathiriwa vibaya na vita ya majimaji na ukandamizaji wake na Wajerumani.

Songea ikaendelea kuwa makao makuu ya mkoa wakati wa uatwala wa Uingereza katika Tanganyika na baada ya uhuru katika Tanzania huria.

MarejeoEdit

  Kata za Wilaya ya Songea Mjini - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania  

Bombambili | Lilambo | Lizaboni | Majengo | Matarawe | Mateka | Matogoro | Mfaranyaki | Misufini | Mjimwema | Mletele | Msamala | Mshangano | Mwengemshindo | Ndilimalitembo | Ruhuwiko | Ruvuma | SeedFarm | Songea Mjini | Subira | Tanga


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Songea (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.