Stefano wa Châtillon

Stefano wa Châtillon (Châtillon-sur-Chalaronne, 1150 - Die, 7 Septemba 1208) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa.

Akitokea familia mashuhuri, alipokuwa na umri wa miaka 25 alijiunga na monasteri ya Wakartusi huko Portes (Bugey).

Kutokana na juhudi zake za pekee katika maisha ya Kiroho, mwaka 1196 alichaguliwa kuwa priori, akaongoza vizuri jumuia yake ya wakaapweke.

Karama zake za uponyaji na utabiri zilimvutia watu wengi waliotaka pia ushauri wake.

Mwaka 1202 alipewa uaskofu, ingawa hakuukubali mpaka alipolazimishwa na papa Inosenti III na mkuu wa shirika.

Pamoja na kuwajibika kwa ajili ya jimbo la Die, na hasa kwa wanyonge, aliendelea kuishi kama Mkartusi kadiri alivyoweza.

Alifariki dunia siku na saa aliyokuwa ametabiri.

Mwaka 1907, Papa Pius X alithibitisha utakatifu wake uliosifiwa tangu zamani.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  • Paul | Guérin | Vie des Saints des Petits Bollandistes| 1876| Bloud et Barral editori | Parigi
  • Piero | Lazzarin | Il libro dei Santi. Piccola enciclopedia| 2007| Edizioni Messaggero | Padova
  • A.| Kleinberg | Storie di santi. Martiri, asceti, beati nella formazione dell'Occidente| 2007| Il Mulino | Bologna
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.