Sumeri

(Elekezwa kutoka Sumer)

Sumeri ilikuwa kati ya tamaduni za juu za kwanza katika Asia ya Magharibi na hasa Mesopotamia (Iraq ya leo). Labda ilikuwa utamaduni wa kwanza wa kujenga miji.

Hati ya Kisumeri inayoonyesha mapatano ya kuuza nyumba na shamba. Maandishi ni mwandiko wa kikabari.

Sumeri ilianzishwa na kuendelea kwenye nchi yenye rutuba kati ya mito Frati na Hidekeli tangu mwaka 3500 KK. Elimu ya akiolojia imeweza kuthibitisha ya kwamba Wasumeri walijenga miji na kuendeleza maandishi.

Maandishi yao yamehifadhiwa kwa sababu waliandika mengi kwa kutumia mwandiko wa kikabari kwenye vigae vya mwandiko wa kikabari, yaani vipande vya udongo mbichi wa ufinyanzi na kuvichoma.

Imetambuliwa pia ya kwamba waliweka misingi muhimu ya kalenda za leo kwa kugawa siku katika saa 24 na saa katika dakika 60. Pia waliweka kumbukumbu ya mifugo na mazao katika maandishi.

Wasumeri waliishi katika dola-miji iliyotawaliwa na wafalme au makuhani.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sumeri kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.