Sinagogi
Sinagogi (au sunagogi) ni nyumba ya dini na ya jamii ya Wayahudi inayotumika hasa kusali.
Etimolojia
haririJina linatokana na neno la Kigiriki συναγωγή syunagoge, likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya neno la Kiebrania בית כנסת beit knesset, yaani "nyumba ya mkutano".
Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.
Muundo
haririChumba kikuu ni ukumbi wa sala lakini mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vinginevyo.
Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:
Historia
haririKatika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.
Baada ya hekalu hilo kujengwa upya, masinagogi yaliendelea kutumiwa na Wayahudi kama nyumba ya kuabudia pia, ila si ya kutolea sadaka za altareni.
Tofauti ni kwamba masinagogi yalikuwa mengi katika Israeli na mahali pote walipoishi Wayahudi nje ya nchi hiyo, lakini kulikuwa na hekalu moja tu duniani, lile la Yerusalemu ambalo kila Myahudi, hata kama alikuwa mbali na mji huo, alipaswa kwenda kuabudu kule wakati wa sikukuu za mwaka.
Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |