Switbati
Switbati (pia: Suitbert, Suidbert, Suitbertus, Swithbert, au Swidbert; Northumbria, Uingereza, 647 hivi – Kaiserswerth, karibu na Dusseldorf, Ujerumani, 1 Machi 713) alikuwa mmonaki Mbenedikto wa Uingereza aliyepata umaarufu kwa kwenda umisionari pamoja na Wilibrodi kati ya makabila ya Ulaya Kaskazini.
Baada ya kupewa daraja ya juu na Wilfrido, alifanya utume huo kama askofu hasa katika Frisia na Westfalia, kati ya Uholanzi na Ujerumani za leo[1].
Mwaka 700 hivi alianzisha monasteri alimofariki.
Anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |