Tabianchi ya Tanzania
Tabianchi ni hali ya mabadiliko ya mazingira upande wa hali ya hewa yaani halijoto, pepo zinazovuma na mvua ambayo yanayojirudia rudia kwa muda mrefu.
Tanzania ni nchi iliyopo mashariki mwa bara la Afrika na imepakana na nchi zifuatazo: upande wa kaskazini imepakana na nchi za Kenya na Uganda, upande wa magharibi imepakana na nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, upande wa kusini kuna nchi za Zambia, Malawi na Msumbiji wakati upande wa mashariki kuna Bahari ya Hindi.
Tabianchi ya Tanzania hubadilika kwa nyakati tofautitofauti katika mwaka.
- Tanzania hupata majira ya joto katika miezi ya Desemba, Januari na Februari. Hata hivyo kiasi cha joto ni cha juu katika ukanda wa Pwani kuliko katika sehemu za nyanda za juu na milimani. Katika miezi hii jua la utosini huwa kwenye kizio cha kusini, hivyo Tanzania hupata joto zaidi.
- Katika miezi ya Juni, Julai na Agosti, kuna hali ya baridi kwa sababu wakati huu jua la utosini huwa katika kizio cha kaskazini.
- Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei ingawa zipo tofauti ndogo kati ya sehemu mbalimbali.
Hivyo kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa.
Mabadiliko ya tabianchi duniani kote yanajitokeza Tanzania pia. Kwa mfano, ongezeko la joto Duniani linasababisha barafuto la mlima Kilimanjaro kuzidi kuyeyuka. Serikali ya nchi imeungana na zile za nchi nyingi kukabili tatizo hilo lakini Kigezo:Bajeti iliyopangwa ni ndogo.
Tazama pia
haririMarejeo
haririVitabu vya Jiografia ya Tanzania
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|