Tarsisi wa Roma (kwa Kilatini: Tarsicius au Tarcisius; alifariki Roma, Italia, 15 Agosti 257) alikuwa mvulana Mkristo aliyeuawa kwa sababu ya imani yake wakati wa kupeleka ekaristi nje ya katakombu palipofanyika ibada[1].

Sanamu ya Mt. Tarsisi, kazi ya Alexandre Falguière (1868).

Kikosi cha Wapagani kilipomsonga ili awaonyeshe sakramenti hiyo, aliona afadhali auawe kuliko kutoa Mwili wa Kristo kwa mbwa[2].

Anajulikana kutokana na shairi la Papa Damaso I aliyemfananisha na Stefano mfiadini.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Agosti[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.