Tennis
Tennis (pia tenisi) ni aina ya michezo inayotekelezwa na watu wawili au wanne wakishindana kwa kupiga mpira mdogo kwa raketi kwenye uwanja wa tennis. Shabaha ni kupiga mpira kwa upande wa mpinzani kwa namna inayomshinda kurudisha mpira. Akishindwa kurudisha mpira upande mwingine mpiganaji wa kwanza anashika pointi moja.
Wanaoshindana ni ama wanaume au wanawake, au timu za mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.
Historia ya michezo
haririChanzo chake kilikuwa wakati wa karne ya 11 huko Ufaransa. Wakati ule wachezaji walipiga kwa mkono wakauita “Jeu de Paume” yaani mchezo wa makofi.
Baada ya kuenea nchini Polandi watu walianza kutumia raketi badala ya makofi. Michezo hii ilipendwa sana Uingereza na Ufaransa.
Jina "tennis" limetokana na neno la Kifaransa "tenez!" linalomaanisha "shika!" au "chukua!".
Katika nusu ya pili ya karne ya 19 imekuwa kati ya michezo ya kupendwa na watu wa tabaka la juu la Uingereza ikasambazwa katika makoloni za Milki ya Uingereza na Marekani. Mashindano makubwa yalianza huko Wimbledon, Uingereza, yanayoendelea hadi leo.
Hadi mwaka 1924 tennis ilikuwa mchezo kwenye Michezo ya Olimpiki, ikaondolewa na kurudishwa mwaka 1988. Katika nchi mbalimbali hadi leo ina sifa ya kuwa mchezo wa matajiri lakini katika nchi nyingine inachezwa na watu wa matabaka yote.
Kuna mashindano makubwa yanayochezwa na timu za taifa yanayojulikana kwa jina la Davis Cup.
Uwanja wa tennis
haririUwanja una umbo la mstatili wenye urefu wa mita 23.77 (futi 78) na upana wa mita 8.23 (futi 27) kwa wachezaji wawili. Kwa wachezaji wanne upana ni mita 10.97 (futi 36).
Katikati ya urefu unatenganishwa kwa wavu kuwa na nusu mbili. Mipaka ya uwanja ni mistari ya nje, wakati mpira unagusa mstari bado uko ndani ya uwanja.
Kuna uwanja wenye mchanga mwekundu (mara nyingi matofali yaliyosagwa), namna ya zulia, chembechembe za plastiki au nyasi, pia nyasi bandia.
Kanuni
haririMchezaji anatakiwa kuangalia ya kwamba
- mpira upite juu ya wavu
- mpira hauruhusiwi kugusa uso wa uwanja zaidi ya mara moja upande wake mwenyewe
- mpira hauruhusiwi kuguswa kwa sehemu yoyote ya mwili
- wavu hautakiwi kuguswa kwa mwili au raketi
- mpira unapigwa mara moja kwa raketi hadi kuutuma upande mwingine
Kukosea hapo kunampa mpinzani pointi.
Refa
haririRefa mkuu anaketi juu ya kiti kirefu akisaidiwa na marefa wa kando.
Picha
hariri-
Mipira
-
Mcheaji wa kike
-
Scoreboard
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- ATP The official site for men's professional tennis
- WTA The official site for women's professional tennis
- Tennis Ball Hopper Ilihifadhiwa 20 Septemba 2017 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Tennis kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |