Theofredi wa Thebe

Theofredi wa Thebe (pia: Chiaffredo, Chiaffredus, Theofredus, Ciafrè, Chaffre, Teofredo, Jafredo, Jafredus, Eufredus, Jofredus, Sinfredus, Zaffredus[1]; alikuwa askari wa jeshi la Roma ya Kale katika kikosi cha Thebe kilichoongozwa na Morisi Mtakatifu[2].

Mchoro mdogo wa Wat. Morisi na Theofredi.

Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi hicho kilijumlisha wanajeshi Waafrika kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo. Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.

Huko Agaunum (leo Saint-Maurice-en-Valais), karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Inasemekana Theofredi alifaulu kukimbia akafia dini huko Crissolo (Piemonte, Italia) [3].

Morisi pamoja na kikosi chake waliheshimiwa mapema kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu ya Theofredi huadhimishwa tarehe 7 Septemba.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Mauritius van Agaunum.
  2. Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography, Literature, Sects and Doctrines (1880), 439.
  3. San Chiaffredo di Saluzzo (Kiitalia)
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.