Theta ni herufi ya nane katika Alfabeti ya Kigiriki. Theta kubwa Θ ina umbo la "O" yenye mstari wa katikati. Theta ndogo θ ina umbo la duaradufu nyembamba pamoja na mstari lala wa katikati lakini kuna pia umbo lisilofungwa kama ϑ.

Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Kwa matumizi ya tarakimu inamaanisha namba 9.[1]

Matamshi yake siku hizi ni sawa na "th" kwa Kiswahili.

Matumizi ya kisayansi

hariri

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na sayansi. Mifano kadhaa ni

 • katika fani ya fizikia
  • Theta ndogo θ au ϑ ni alama ya halijoto
  • Theta ndogo ni alama kwa kiwango cha pembe katika usokotaji.
  • Theta kubwa Θ hutumiwa kama alama ya kuonyesha nguvu ya uga magnetiki
 • katika fani ya astronomia
  • Theta kubwa Θ inataja saa za nyota
  • Theta ndogo ϑ hutaja nyota inayoonekana kwenye nafasi ya tisa katika kundinyota kulingana na nguvu ya nuru yake.

Marejeo

hariri
 1. Theta ina maana ya tisa ingawa siku hizi ni herufi ya nane. Sababu yake ni ya kwamba alama ya digamma imepotea katika alfabeti lakini imebaki kama tarakimu ya sita