Tau (Τ τ) ni herufi ya 19 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama τ (alama ya kawaida) au Τ (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu ikiwa alama ya namba 300.

Tau uc lc.svg
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma uc lc.svg Digamma 6 San uc lc.svg San 90
Stigma uc lc.svg Stigma 6 Sho uc lc.svg Sho 90
Heta uc lc.svg Heta 8 Qoppa uc lc.svg Koppa 90
Sampi uc lc T-shaped.svg Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Asili ya tau ni herufi ya Kifinisia "taw" Phoenician taw.svg (𐤕). Herufi zilizotokana nayo katika alfabeti zilizofuata Kigiriki ni T katika alfabeti ya Kilatini na Te (Т, т) katika alfabeti ya Kikirili.

Matamshi yake ilikuwa "t".

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, τ inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hisabati na fizikia.