Kappa ni herufi ya kumi katika Alfabeti ya Kigiriki. Umbo la kappa kubwa na ndogo limeendelea vilevile katika alfabeti ya Kilatini na hivyo hutumiwa vile hadi leo katika lugha zote zinazotumia mwandiko huo kama vile Kiswahili, Kiingereza na kadhalika. Matamshi yake ni "K", sawa na Kiswahili.

Kappa uc lc.svg
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma uc lc.svg Digamma 6 San uc lc.svg San 90
Stigma uc lc.svg Stigma 6 Sho uc lc.svg Sho 90
Heta uc lc.svg Heta 8 Qoppa uc lc.svg Koppa 90
Sampi uc lc T-shaped.svg Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Kwa matumizi ya tarakimu inamaanisha namba 20.

Kama neno lenye asili ya Kigiriki limepokelewa katika lugha ya Kiingereza mara nyingi herufi "C" imechukua nafasi ya "K". Sababu yake ni kwamba Waroma waliandika "k" mara nyingi kama "c" katika Kilatini maana hawakutofautisha herufi hizi mbili.

Matumizi ya kisayansiEdit

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, kappa inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na sayansi.

MarejeoEdit