Dzeta (pia: Zeta) ni herufi ya sita katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama ζ (alama ya kawaida) au Ζ (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu, ikiwa alama ya namba 7.

Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Asili ya dzeta ni herufi ya Kifinisia ya zayin (tazama makala ya herufi Z). Matamshi yake yalikuwa "dz", katika Kigiriki cha kisasa ni zaidi kama Z ya Kiswahili. Kutokana na herufi hiyo, alfabeti ya Kilatini ina "Z" na alfabeti ya Kikirili ina "З".

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki ζ inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hisabati na fizikia.