Delta ni herufi ya nne ya Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa Δ (herufi kubwa ya mwanzo) au δ (herufi ndogo ya kawaida).

Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Katika Ugiriki ya Kale ilihesabiwa pia kama namba "4".

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za Kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fisikia. Inaweza kutumiwa kutaja pembe ya nne katika pembenne.

Katika astronomia inatumiwa kuanza hesabu ya nyota katika kundinyota. Katika mfumo wa Bayer inataja nyota angavu ya nne katika kundinyota fulani.

Asili ya delta ni herufi ya kifinisia ya daleth (tazama makala ya D). Matamshi yake ni kama D ya Kiswahili.