Thule ilikuwa jina la kisiwa kwenye Atlantiki upande wa kaskazini wa Ulaya kilichotajwa na Pytheas wa Massilia, mpelelezi wa Ugiriki ya Kale katika karne ya 4 KK[1].

Haijulikani ni kisiwa gani alichotaja kama kilikuwa Iceland, Greenland au labda visiwa vya Faroe. Kuna hakika ya kwamba Pytheas alitaja mahali pa kaskazini kwa sababu aliandika ya kwamba "bahari inayoganda", yaani bahari inayofunikwa na barafu, ilianza safari ya siku 1 kutoka kule. Lakini haijulikani aliandika katika mwezi gani na uenezaji wa barafu baharini unabadilika pamoja na majira.

Kwa hiyo jina la Thule lilitumiwa katika Ulaya kwa kutaja mwisho wa Dunia iliyoweza kufikiwa na watu kabla ya kuingia katika maeneo ya barafu tupu.[2]

Kutokana na imani hii jina la "Ultima Thule", ambalo ni Kilatini kwa "Thule ya mwisho" limekuwa namna ya kutaja "mwisho wa Dunia".

Katika mwezi wa Machi 2018 NASA iliamua kuita kiolwa cha angani katika Ukanda wa Kuiper "Ultima Thule" kwa sababu ni kiolwa cha mbali kabisa kitakachotembelewa na kipimaanga New Horizon mnamo tarehe 1 Januari 2019[3]. Mnamo mwaka 2019 Umoja wa Kimataifa wa Astronomia uliamua jina rasmi kuwa "Arrokoth".

Kujisomea

hariri
  • Burton, Richard F. (1875). Ultima Thule: Or, A Summer in Iceland. London, Edinburgh: W.P. Nimmo. Downloadable Google Books.
  • Fotheringham, W.H. (1862). "On the Thule of the Ancients" (pdf). Proceedings of the Society of Antiquaries of Scotland. III: 491–503.
  • Gilberg, Rolf (Juni 1976). "Thule" (PDF). Arctic. 29 (2): 83–86. doi:10.14430/arctic2793. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pfd) mnamo 2011-05-24. Iliwekwa mnamo 2008-10-30. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Joanna Kavenna, The Ice Museum: In Search of the Lost Land of Thule, London, Penguin, 2006. ISBN 978-0-14-101198-1
  • Pliny (1829). Histoire naturelle de Pline: Traduction Nouvelle: Vol III (kwa French). Ajasson de Grandsagne (trans.). Paris: C.L.F. Panckoucke. ku. 337–338, notes on Book IV.{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  • Pliny (1893). The Natural History of Pliny: Volume I. Ilitafsiriwa na John Bostock; Henry Thomas Riley. London, New York: George Bell & Sons. ku. 352, notes on Book IV.
  • Thule, makala ktk Encyclopedia Britannica 1911

Viungo vya nje

hariri
  1. [1], STRABO, Geographica, 2.4.1. (trans. HAMILTON, H.C. and FALCONER, W.)
  2. [2] Ilihifadhiwa 26 Desemba 2018 kwenye Wayback Machine., tovuti ya "Idols of the Cave" inayokusanya habari nyingi kuhusu Thule na maana mbalimbali za jina hili
  3. New Horizons Chooses Nickname for ‘Ultimate’ Flyby Target, tovuti ya NASA, 3 Machi 2018
  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.