Tingatinga (uchoraji)

(Elekezwa kutoka Tingatinga (painting))

Tingatinga (pia huandikwa Tinga-tinga au Tinga Tinga) ni mtindo wa uchoraji ulioanzishwa mnamo mwaka 1970's katika eneo la Masaki jijini Dar es Salaam (Tanzania) na baadaye kuenea katika sehemu kubwa ya Afrika Mashariki. Mtindo huo umepewa jina la mwanzilishi wake, mchoraji wa Kitanzania Edward Said Tingatinga. Picha za aina hiyo zinalenga hasa soko la watalii na wageni kwa jumla. Picha hizi za Tinga Tinga zimehamasisha utengenezaji wa katuni za watoto iitwayo Tinga Tinga Tales[1][2]

Punda Milia Baba na Mama - uchoraji kwa mtindo wa Tingatinga na Rubuni Rashidi Said (2021)
Wachoraji wa Tingatinga jinsi walivyoanza kuuza kazi zao huko Oyster Bay, Dar es Salaam. Picha ya mwaka 1973.

Mwanzoni picha za Tingatinga zilichorwa kwenye hadibodi iliyopatikana kwa bei nafuu, kwa kutumia rangi ya baisikeli. Rangi zilizotumiwa ni zile zinazong'aa. Fomati ya picha ilikuwa mraba, maana ilikuwa njia ya kutumia vipande vya hadibodi vilivyopatikana bila kuacha mabaki.

Picha zilichorwa kwa soko la watalii na Wazungu waliofanya kazi nchini, maana walikuwa wenye pesa na tayari kutoa pesa kwa sanaa. Kwa hiyo picha nyingi zinaonyesha wanyama walio mashuhuri kama "wakubwa watano", yaani simba, chui, kifaru, ndovu na nyati wanaotafutwa zaidi na watalii, pamoja na wanyama wengine wanaoonekana kwenye mbuga za wanyama.

Historia

hariri

Mwanzilishaji wa mtindo huo alikuwa Edward Tingatinga aliyeanza kuchora mnamo 1968 mjini Dar es Salaam. [3] Alitumia vifaa vya gharama nafuu kama vile hadibodi na rangi ya baisikeli akafaulu kuvuta watalii kununua kazi yake. Mwenyewe hakuchora wanyama pekee, lakini pia watu pamoja na wanyama na pia "masheitani" kufuatana na utamaduni wa Wamakonde[4].

Tingatinga alipouawa mwaka wa 1972, mtindo wake ulikuwa maarufu tayari, alikuwa na kundi la wanafunzi wake walioitwa "shule ya Tingatinga" kwa njia isiyo rasmi. [5]

Kizazi cha kwanza cha wasanii waliomfuata Tingatinga, walirudia tu mtindo wake. Lakini katika miaka iliyofuata, wachoraji walipanua chaguo la motifu yaani vitu walivyoonyesha katika picha zao, kama vile msongamano wa watu kwenye masoko ya mjini, au kwenye daladala (au matatu), pamoja na kutumia mitindo mipya kama vile mtazamo wa kisanii.

Mmoja wa wachoraji wa Tingatinga wa kizazi cha pili anayejulikana sana ni shemeji wa Edward Tingatinga, Simon Mpata.

Edward Tinagatinga mwenyewe aliacha idadi ndogo tu ya picha za kuchora, ambazo siku hizi hutafutwa na wakusanyaji. Michoro yote maarufu ya Tingatinga, kama vile Simba, Tausi kwenye Mti wa Mbuyu, Antelope, Chui, Nyati, au Tumbili ilinakiliwa na kuuzwa mara nyingi kwa jina lake, kumbe ni bandia. [6]

 
Chui, na Rubuni

Siku hizi wachoraji wengi wa mtindo wa Tingatinga hutumia rangi za mafuta kwenye kitambaa.

Chama cha Ushirika cha Tingatinga

hariri

Baada ya kifo cha ghafla cha Edward Tingatinga, wanafunzi wake 6 wa moja kwa moja waliokuwa Ajaba Abdallah Mtalia, Adeusi Mandu, January Linda, Casper Tedo, Simon Mpata, na Omari Amonde [7] walijaribu kujipanga upya. Jamaa wa Tingatinga nao walijiunga na kundi hili ambalo baadaye liliitwa "Tingatinga (au Tinga Tinga) Partnership". Sio wafuasi wote wa Tingatinga waliokubali kuwa katika kundi hilo; wengine waliunda kikundi kipya huko Slipway, Masaki. [8] Mnamo 1990, Ushirikiano wa Tingatinga ulijiunda na kuwa shirika lilipewa jina la Tingatinga Arts Cooperative Society (TACS). [9]

Shirika hili limeunda tovuti yake mnamo Mei 2018: www.tingatingaArt.com

Marejeo

hariri
  1. "Tinga Tinga Tales", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-04-08, iliwekwa mnamo 2023-05-14
  2. "File:Tinga Tinga Tales.png", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2020-09-29, iliwekwa mnamo 2023-05-14
  3. "Tinga Tinga art". Tingatinga.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-05-12. Iliwekwa mnamo 2013-09-30.
  4. https://www.africancontemporary.com/Edward%20Saidi%20Tingatinga%20gallery.htm
  5. The tingatinga school of painting. This is an informal term (i.e., those who paint after Tingatinga's example) and not to be confused with the Tingatinga Arts Cooperative Society, which is a specific organization, although sometimes also referred to as a "school". "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Septemba 2010. Iliwekwa mnamo 2010-01-10.{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link) CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Are Tingatinga fakes a problem today?". Alexdrummerafrica.blog.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Machi 2012. Iliwekwa mnamo 2013-09-30.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Mwasanga, National Arts Council, Mture Publishers, Tingatinga, p 30
  8. Abdellahamani Hasani
  9. "Tingatinga Co-operative Society". Tingatinga.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-28. Iliwekwa mnamo 2013-09-30.

Kujisomea zaidi

hariri
  • Tingatinga. 1998. ISBN 978-9976-967-34-0.
  • "The Authenticity of Today's Tingatinga Art". 
  • Thorup, Tine; Sam, Cuong (2011). Tingatinga Kitch Or Quality Bicycle Enamel on Board & Canvas. ISBN 978-87-992635-2-3.

Viungo vya nje

hariri