Tongoni

Tongoni ni jina la kata iliyopo ndani ya eneo la Jiji la Tanga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania yenye Postikodi namba 21207. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 4,594 [1] waishio humo.

Tongoni iko takriban kilomita 14 upande wa kusini wa kitovu cha jiji kando ya barabara inayokwenda Pangani, ikitazama Bahari Hindi.

Ni mahali pa kihistoria jinsi inavyoonekana kwenye magofu ya Tongoni yenye msikiti na takriban makaburi 20.[2] Takriban miaka 600 iliyopita kulikuwepo hapa mji wa Tangata (pia: Mtangata) iliyokuwa mahali muhimu pa biashara. Mahali pake kwenye mdomo mpana wa mto unaoishia hapa palileta nafasi salama ya kutia nanga kwa jahazi. Inasemekana ya kwamba nahodha Mreno Vasco da Gama alipumzika hapa kidogo wakati wa safari yake ya kwanza kuelekea Bara Hindi mnamo mwaka 1498. Magofu ni pamoja na msikiti na makaburi yenye nguzo jinsi ilivyokuwa kawaida kwenye makaburi ya Waswahili.[3]

Magofu ya TongoniEdit

MarejeoEdit

  1. Sensa ya 2012, Tanga - Tanga CC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
  2. Tongoni Ruins, tovuti ya Lonely Planet, iliangaliwa Septemba 2018
  3. Briggs, McIntyre ukurasa 372

VitabuEdit

  • Philip Briggs, Chris McIntyre: Tanzania Safari Guide: With Kilimanjaro, Zanzibar and the Coast, Bradt Travel Guides 2013, ISBN-10: 9781841624624, ISBN-13: 978-1841624624ISBN
  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tongoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
  Kata za Wilaya ya Tanga - Tanzania  

CentralChongoleaniChumbageniDugaKangeKaseraKiomoniKirareMabawaMabokweniMagaoniMajengoMakororaMarunguMasiwaniMaweniMnyanjaniMsambweniMwanzangeMzinganiMzizimaNgamiani KaskaziniNgamiani KatiNgamiani KusiniNguvumaliPongweTangasisiTongoniUsagara