Kinyama-bapa

(Elekezwa kutoka Trichoplacidae)
Kinyama-bapa
Trichoplax adhaerens chini ya hadubini
Trichoplax adhaerens chini ya hadubini
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia
Faila: Placozoa
Familia: Trichoplacidae
Bütschli & Hatschek, 1905
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 3:

Vinyama-bapa ni aina za msingi za viumbehai vya bahari (visivyo vimelea) vyenye seli nyingi. Wana muundo sahili sana wa wanyama wote. Kufikia sasa, jenasi tatu, kila moja na spishi moja, zimepatikana: Trichoplax adhaerens, Hoilungia hongkongensis na Polyplacotoma mediterranea, ambapo ile ya mwisho huonekana msingi zaidi. Mbili za mwisho zimepatikana tu tangu 2017. Ingawa spishi ya kwanza iligunduliwa mnamo 1883 na mwanazoolojia wa Ujerumani Franz Eilhard Schulze (1840-1921) na tangu miaka ya 1970 ilichambuliwa zaidi na mtaalamu wa protozoolojia wa Ujerumani Karl Gottlieb Grell (1912-1994), jina la kawaida bado halipo kwa faila hii katika takriban lugha zote.

Maelezo

hariri

Vinyama-bapa ni wanyama wadogo waliokuwa bapa wenye kipenyo cha hadi mm 1. Kama amiba hawana kivimbe laini, ingawa uso wa chini umebonyea kidogo na uso wa juu huwa bapa. Mwili una tabaka la nje la epiteli sahili lililozunguka karatasi ya seli za nyota zinazofanana na mesenkimi ya wanyama wengine tata zaidi. Seli za epiteli hubeba silio (nywele ndogo sana) ambazo wanyama hao hutumia kuwasaidia kutambaa kwenye sakafu ya bahari.

Uso wa chini humeza chembe ndogo za takataka ogania, ambayo wanyama hula. Huzalisha kinafsia wakichipua violezo vidogo na uso wa chini pia unaweza kuchipua mayai katika mesenkimi.

Uzazi wa kijinsia umeripotiwa kutokea katika spishi moja. Uunganishaji baini ya jeni ulionekana na vile vile sifa nyingine za uzazi wa kijinsia.

Spishi kadhaa zina vijidudu vya Rickettsiales vinavyoishi ndani ya mwili wao. Angalau spishi moja iliibuka kuwa na spishi mbili za bakteria ndani yake. Grellia, anayeishi katika retikulamu ya endoplasma ya mnyama huyu, anachukuliwa kuwa na jukumu katika uzalishaji wa protini na utando wa seli. Kijidudu kingine ni Margulisbacteria ilivyoelezwa kama spishi ya kwanza ambayo huishi ndani ya seli na hutumiwa kwa mmeng'enyo wa miani. Inaonekana kula mafuta na lipidi nyingine za miani na kumpa mwenyeji wake vitamini na asidi amino kwa kurudi.