Ujenzi wa taifa ni mchakato wa kujenga au kuunda utambulisho wa kitaifa kwa kutumia nguvu ya serikali. Utaratibu huu unalenga kuunganisha wananchi katika taifa ili ibakie imara kisiasa katika kipindi kirefu. Ujenzi wa taifa unaweza kuhusisha matumizi ya propaganda au maendeleo makubwa ya miundomsingi ili kuendeleza matabaka ya kijamii na ukuaji wa uchumi.

Hapo awali, ujenzi wa taifa ulifahamika kama juhudi za mataifa mapya huru kujitegemea, hasa mataifa ya Afrika yaliyoundwa na wakoloni bila kufikiria mipaka ya kikabila wala mambo mengine.[1] [2]

Ujenzi wa taifa ulijumuisha uumbaji wa parafanalia ya juu ya taifa kama vile bendera, nyimbo za taifa, sikukuu za kitaifa, viwanja vya kitaifa, mashirika ya ndege ya kitaifa, lugha za taifa na hadithi za kitaifa. Katika ngazi ya ndani, utambulisho wa kitaifa ulihitajika kujengwa kwa kusudi la kuunganisha makundi mbalimbali kuwa taifa, hasa ukoloni ulipokuwa ukitumia mbinu za kugawanya na kutawala ili kudumisha utawala wake.

Hata hivyo, mataifa mengi mapya yalikumbwa na "ukabila", migogoro kati ya makundi ya kikabila ndani ya taifa. Wakati mwingine, jambo hili lilikaribia kusababisha kusambaratika kwao, kama vile jaribio la Biafra kujitenga kutoka Nigeria mwaka wa 1970, au Wasomali katika kanda ya Ethiopia ya Ogaden kutaka uhuru kamili. Barani Asia, utengano wa India, Pakistan na Bangladesh ni mfano mwingine ambapo tofauti ziligawanyisha taifa la baada ya ukoloni. Mauaji ya halaiki ya Rwanda na vilevile matatizo yaliyoikumba Sudan na Sudan Kusini mara kwa mara yanaweza kuhusishwa na ukosefu wa mshikamano wa kikabila au wa kidini katika nchi. Imethibitika ni vigumu kuunganisha mataifa yenye asili sawa za kikabila lakini tofauti za kikoloni. Mfano wa kushindikana kwa Shirikisho la Senegambia na matatizo ya Kamerun vinaonyesha ugumu wa kuunganisha maeneo yanayotumia lugha ya Kiingereza na yanayotumia lugha ya Kifaransa.

Kumekuwepo utatanishi kati ya matumizi ya neno ujenzi wa taifa na lile la ujenzi wa serikali (maneno haya mara nyingine hutumika kama jina moja katika Amerika Kaskazini). Yote yana maana finyu na tofauti katika sayansi ya kisiasa, la kwanza likimaanisha utambulisho wa kitaifa, na la pili taasisi za serikali. Mjadala huu umefanywa mgumu zaidi kwa kuwepo kwa makundi mawili ya mawazo juu ya ujenzi wa serikali. La kwanza (limeenea katika vyombo vya habari) huonyesha ujenzi wa serikali kama kitendo kinachoingiliwa na nchi za kigeni. La pili (asili ya kitaaluma lakini linaendelea kukubaliwa na taasisi za kimataifa) huona ujenzi wa serikali kama mchakato wa kiasili.

Utatanishi juu ya maneno hayo ina maana kuwa hivi majuzi, ujenzi wa taifa umekuja kutumika katika mazingira tofauti kabisa, ukirejelewa vile lilivyoelezewa na wapinzani wake kama "matumizi ya silaha katika wa migogoro ya kuelekea demokrasia". Katika maana hii ujenzi wa taifa, bora likijulikana kama ujenzi wa serikali, linaelezea juhudi za kimakusudi za nguvu ya kigeni kujenga au kuweka taasisi ya serikali ya kitaifa, ikizingatia mfano unaoweza kuwa sawa na wake lakini mara nyingi hufikiriwa kuwa ya kigeni na hata inayoleta farakano. Katika maana hii, ujenzi wa serikali kwa kawaida huonekana kwa uwekezaji mkubwa, uvamizi wa kijeshi, serikali ya mpito, na matumizi ya propaganda kuwasilisha sera za serikali.

Marejeo

hariri
  1. "^ Economic Development & Nation-building in Africa: In Search of A New Paradigm". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-30. Iliwekwa mnamo 2018-09-03.
  2. Nation-Building, Propaganda, and Literature in Francophone Africa

Viungo vya nje

hariri
  • Fritz V, Menocal AR, Understanding State-building from a Political Economy Perspective, ODI, London 2007
  • CIC/IPA, Concepts and Dilemmas of State-building in Fragile Situations, OECD-DAC, Paris, 2008
  • Whaites, Alan, State in Development: Understanding State-building, DFID, London 2008
  • Engin, Kenan: 'Nation-Building' - Theoretische Betrachtung und Fallbeispiel: Irak, Nomos Verlag, Baden Baden 2013, ISBN 978-3-8487-0684-6