Wilaya ya Ukerewe

(Elekezwa kutoka Ukerewe)

Wilaya ya Ukerewe ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Mwanza.

Mahali pa visiwa vya Ukerewe (kijani kilichokoza) katika mkoa wa Mwanza kabla ya kumegwa.

Eneo la wilaya hiyo liko kwenye visiwa vya ziwa Viktoria Nyanza, hasa visiwa viwili vikubwa vya Ukerewe na Ukara pamoja na visiwa vidogo kama vile Kweru, Goziba, Sizu, Irugwa, Kerebe na vingine vingi.

Wakazi

hariri

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 261,944 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 387,815 [2].

Wilaya ya Ukerewe ina makabila makuu matatu ambayo ni Wakerewe, Wakara na Wajita. Kabila kuu zaidi ni la Wakerewe ambalo ndilo jina la kisiwa kikuu pia. Wakara wanapatikana nje kidogo ya kisiwa hicho katika kisiwa cha Ukara. Halafu kuna Wajita ambao asili yao ni mkoa wa Mara.

Watu maarufu

hariri

Ukerewe umewahi kutoa viongozi wakubwa serikalini kama Pius Msekwa, spika wa bunge mstaafu, Gertrude Mongella na wengine wengi. Pia uliwahi kutoa padri wa kwanza mzawa wa Kanisa Katoliki aliyeitwa padri Chipanda lakini pia ni eneo lililojengwa ghorofa la kwanza na mtu Mweusi.

Usafiri

hariri

Usafiri ni wa aina kuu mbili: usafiri wa majini na wa ardhini ambao huwarahisishia wakazi wa eneo hili kufanya kazi na shughuli mbalimbali za maendeleo katika wilaya yao.

Uchumi

hariri

Ukerewe unasifika kwa kutoa matunda aina ya machungwa ambayo wananchi wake huyatumia kula na kama biashara ili kujiongezea kipato.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Kata za Wilaya ya Ukerewe - Mkoa wa Mwanza - Tanzania  

BukandaBukikoBukindoBukongoBukunguBwiroBwisyaIgallaIlangalaIrugwaKageraKagunguliKakeregeKakukuruMukituntuMuritiMurutunguruNakatunguruNamagondoNamilembeNansioNdurumaNgomaNkilizyaNyamanga

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Ukerewe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.