Umaksi (pia: Umarksi, Umarx, kwa Kiingereza Marxism) ni falsafa ambayo inafuata uyakinifu na inakusudia kuleta maendeleo ya haraka katika jamii kuanzia uchumi unaotazamwa kuwa msingi wa mahusiano yote.

Karl Marx

Lengo kuu ni kuondoa matabaka katika jamii na kuleta usawa katika ya binadamu. Njia ni kuwawezesha wanyonge kudai haki zao kwa kuungana na kuleta mapinduzi dhidi ya wanyonyaji.

Katikati ya karne ya 19, waanzilishi wa jitihada hizo walikuwa Wajerumani wawili: Karl Marx na Friedrich Engels. Jina Umaksi linatokana na wa kwanza kati yao, Marx.

Umaksi uliendelezwa na watu mbalimbali hasa katika karne ya 20 kadiri siasa hiyo ilivyozidi kuenea duniani, hadi kuongoza maisha ya theluthi ya binadamu wote. Kati yao, Vladimir Ilich Lenin, Leon Trotsky, Joseph Stalin nchini Urusi na Mao Zedong huko China. Katika Umoja wa Kisovyeti na nchi zilizotawaliwa na Wakomunisti mabadiliko ya fundisho hili yaliitwa Umaksi-Ulenin (Marxism-Leninism) na kuwa itikadi rasmi.

Baada ya ukomunisti kushindikana Ulaya Mashariki pamoja na Urusi kusambaratika (1989), mvuto wa falsafa hiyo umepungua sana.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: