Josef Stalin

(Elekezwa kutoka Stalin)

Joseph Vissarionovich Stalin (kwa Kirusi: Иосиф Виссарионович Сталин, Iosif Vissarionovich Stalin; jina la kiraia: Джугашвили, Dzhugashvili, kwa Kigeorgia: იოსებ ჯუღაშვილი, Ioseb Jughashvili; 18 Desemba (katika Kalenda ya Juliasi: 6 Desemba) 18785 Machi 1953) alikuwa mwanasiasa wa Urusi kutoka Georgia aliyeshiriki pamoja na Lenin katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 na kuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti halafu kiongozi mkuu wa Umoja wa Kisovyeti baada ya kifo cha Lenin.

Josef Stalin mwaka 1942.

Alitawala Urusi kama dikteta kwa unyama na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu. Alifaulu kujenga uchumi na jeshi la Umoja wa Kisovyeti na kutetea nchi dhidi ya mashambulio ya Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Alikuwa kati ya washindi wa Vita Kuu ya Pili akapanua utawala wake juu ya nchi za Ulaya ya Mashariki na ya Kati kama vile Poland, Ucheki, Hungaria, Romania, Bulgaria na sehemu ya mashariki ya Ujerumani.

Stalin alikubaliwa kama kiongozi wa nchi zote za kikomunisti pamoja na China, Vietnam na Korea ya Kaskazini hadi kifo chake.

Alifuatwa na Nikita Krushchov kama kiongozi wa chama na Umoja wa Kisovyeti.

Joseph Stalin alikuwa na wake wawili kwa vipindi tofauti: mke wa kwanza aliitwa Ekaterine Svanidize (1906-1907), na wa pili aliitwa Nadezhda Alliluyeva (1919-1932). Pia alikuwa na watoto watatu walioitwa Yakov Dzhugashvilli, Vasily Dzhugashvilli na Svetlana Alliluyeva.

Jina la utani la Joseph Stalin lilikuwa ni 'Koba'.

Crystal personal.svg Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Josef Stalin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.