Utitiri-mahameli mkubwa
Utitiri-mahameli mkubwa | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Utitiri-mahameli mkubwa
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
|
Utitiri-mahameli mkubwa (Dinothrombium tinctorium) ni utitiri mkubwa wa familia Trombidiidae katika oda Trombidiformes ambaye ni baini ya spishi kubwa kabisa za matitiri (hadi mm 12).
Maelezo
haririUtitiri huyu ni mkubwa: mm 10-12, na ana rangi ya nyekundu kali. Ana miguu minane kama arakinida wote. Mwili umegawanywa katika gnathosoma na idiosoma kama matitiri wengine na pia umefunikwa kwa manyoya mengi kama mahameli.
Makazi
haririSpishi hii hutokea maeneo ya jangwa na nusujangwa. Hatua zote za spishi hii huishi katika mchanga au ndani ya takataka za mimea na huonekana nadra. Wapevu hutokea baada ya mvua kubwa na kwa hivyo huitwa “rain bugs” (wadudu-mvua) kwa Kiingereza.
Mzunguko wa maisha
haririJike anaweza kutaga mayai 100,000. Hatua ya kwanza inayotoka katika yai inaitwa pre-larva (hatua kabla ya lava), kisha kuna hatua moja ya lava, hatua tatu za tunutu (protonymph, deutonymph na tritonymph) na hatua ya mpevu. Pre-larva, protonymph na tritonymph hawana kinywa na miguu ni midogo sana au haiko. Lava ni vidusia wa nje juu ya arithropodi kama panzi, mbawakawa, vipepeo, buibui na buingamia. Deutonymph na wapevu ni mbuai wa arithropodi. Mbuawa wanaopendelewa na wapevu ni kumbikumbi.
Utetezi dhidi ya maadui
haririRangi ya matitiri hao ni nyekundu kali kama onyo kwa maadui. Yaani wana ladha mbaya.