Utitiri (Arithropodi)
Utitiri | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kifani cha utitiri mwekundu wa kuku
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Oda za juu 3 na oda 6:
|
Kwa asili jina utitiri hutumika kwa ugonjwa wa kuku ambao unasababishwa na wadudu wadogo walio na mnasaba na kupe na papasi. Lakini kwa sababu hakuna jina la jumla la Kiswahili kwa kundi la Acari “utitiri” hutumika zaidi na zaidi kwa spishi nyingine za Acari. Kwa asili pia neno hili lilikuwa nomino isiyoweza kuhesabiwa, kama sukari kwa mfano, lakini watu wengine wameanza kulichukulia kama neno katika umoja (pengine hata titiri) na "matitiri" kama wingi. Utitiri ni nusungeli katika ngeli ya Arachnida. Kwa hivyo wana miguu minane kama buibui na nge.
Utitiri ni arithropodi wadogo. Spishi kubwa kabisa zina mm 10-20, lakini takriban spishi zote ni ndogo au ndogo sana: spishi ndogo kabisa ina mm 0.05. Utitiri ni tele katika udongo ambapo husaidia kumeng'enya dutu ya viumbehai. Lakini spishi zinazojulikana zaidi ni vidusia vya nje vya wanyama na mimea. Mifano ya vidusia ni kupe, papasi, funduku na utitiri mwekundu.
Maelezo
haririKwa kiasili mwili wa matitiri uligawanywa katika sehemu mbili zenye pingili, kama arakinida wengine: prosoma (kefalotoraksi) na opisthosoma (fumbatio). Walakini dalili dhaifu sana za pingili zinabaki katika matitiri. Prosoma na opisthosoma zimeungana na mahali pa ganda kinamo (bopo llinalozunguka kichwa) hutenganisha kelisera na pedipalpi kutoka mwili. Sehemu hii ya mbele ya mwili huitwa gnathosoma. Sehemu iliyobaki ya mwili huitwa idiosoma na ni ya kipekee katika matitiri.
Matitiri wapevu wengi wana jozi nne za miguu, lakini wengine wana michache zaidi. Kwa mfano, matitiri-kinundu, kama Phyllocoptes variabilis (familia Eriophyidae), wana mwili kama mnyoo wenye jozi mbili tu za miguu. Baadhi ya matitiri vidusia wana jozi moja au tatu za miguu katika hatua ya mpevu. Hatua za lava hazina zaidi ya jozi tatu za miguu. Matitiri wapevu walio na jozi tatu tu za miguu wanaweza kuitwa “larviform” (umbo la lava). Pia, wana wa Nematalycidae ndani ya Endeostigmata, ambao huishi kati ya chembe za mchanga, mara nyingi huwa na miili iliyorefuka kama minyoo yenye miguu michache.
Sehemu za kinywa za matitiri zinaweza kutoholewa kwa kung'ata, kudunga, kukeketa au kufyonza. Wanapumua kupitia spirakulo, trakea, matumbo na ngozi yenyewe. Spishi zinazowinda matitiri wengine zina hisi nyepesi, lakini matitiri wengi hawana macho. Macho ya katikati ya arakinida hayapatikani au huungana katika jicho moja. Kwa hivyo, idadi yoyote ya macho kutoka moja hadi matano inaweza kutokea.
Spishi zilizochaguliwa za Afrika
hariri- Acariformes
- Sarcoptiformes
- Astigmata
- Sarcoptes scabiei (Linnaeus, 1758), Funduku
- Astigmata
- Trombidiformes
- Prostigmata
- Brevipalpus phoenicis (Geijskes, 1939), Utitiri bapa wa mchai
- Dinothrombium tinctorium (Linnaeus, 1767), Utitiri-mahameli mkubwa
- Mononychellus tanajoa (Bondar, 1938), Utitiri kijani wa muhogo
- Oligonychus coffeae (Nietner, 1861), Utitiri mwekundu wa mbuni
- Polyphagotarsonemus latus (Banks, 1904), Utitiri mpana
- Tetranychus evansi Baker & Pritchard, 1960, Utitiri-utando mwekundu
- Tetranychus urticae C.L. Koch, 1836, Utitiri-utando madoa-mawili
- Prostigmata
- Sarcoptiformes
- Opilioacariformes
- Opilioacaridae
- Opilioacarus segmentatus With, 1902
- Panchaetes dundoensis Naudo, 1963
- Panchaetes papillosus (André, 1947)
- Opilioacaridae
- Parasitiformes
- Mesostigmata
- Amblyomma variegatum (Fabricius, 1794), Kupe wa ng'ombe
- Amblyseius andersoni (Chant, 1957), Utitiri-mbuai
- Dermanyssus gallinae (De Geer, 1778), Utitiri mwekundu wa kuku
- Ornithodoros moubata Murray, 1877, Papasi wa homa ya vipindi
- Ornithodoros savignyi (Audouin, 1827), Papasi-mchanga
- Phytoseiulus persimilis Athias-Henriot, 1957, Utitiri-mbuai
- Rhipicephalus appendiculatus Neumann, 1901, Kupe-masikio kahawia
- Mesostigmata
Picha
hariri-
Funduku katika ngozi
-
Utitiri bapa wa mchai
-
Utitiri-mahameli mkubwa
-
Utitiri mpana
-
Utitiri-utando madoa-mawili
-
Kupe wa ng'ombe aliyejaa na damu
-
Utitiri-mbuai
-
Papasi wa homa ya vipindi
-
Papasi-mchanga
-
Utitiri-mbuai
-
Kupe-masikio kahawia