Uwanja wa michezo wa Free State
Uwanja wa michezo wa Free State kwa sasa unatambulika kama Uwanja wa Toyota kwa masuala ya ufadhili na hapo zamani ilifahamika kama (Vodacom Park). Ni uwanja unaopatikana Bloemfontein, Afrika Kusini na unatumika mahususi kwa ajili ya mchezo wa raga na mara nyingine hutumika kwa ajili ya michezo ya soka. Ilitengenezwa mnamo mwaka 1995 kwa ajili ya kombe la dunia la raga na ilikuwa moja ya viwanja vilivyotumika kwa kombe la dunia la FIFA mwaka 2010.
Watumizi wapangaji wa msingi wa uwanja huu kwa mchezo wa raga ni wafuatao:
- Cheetahs umoja wa raga wanao wakilisha jimbo la Free state na ghuba ya kaskazini katika mashindano ya kimataifa ya Pro14.
- Free State Cheetahs, washiriki wa kombe la ndani la Currie.
Watumiaji (wapangaji) wa msingi wa shirikisho la mpira wa miguu katika uwanja huu ni:
- Klabu ya Bloemfontein Celtic F.C wanaocheza ligi ya ndani ya Afrika Kusini.
Kombe la dunia la raga ya 1995
haririIlikuwa miongoni mwa viwanja vilivyotumika kwa kombe la dunia la raga ya mwaka 1995. Mzunguko wote wa kwanza wa kundi C ulichezwa katika uwanja huu.
Tarehe | Timu #1 | Matokeo. | Timu #2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|
27 Mei 1995 | Japan | 10–57 | Wales | Kombe la Dunia la raga kundi C | 12,000 |
31 Mei 1995 | Ireland | 50–28 | Japan | Kombe la dunia la raga kundi C | 15,000 |
4 June 19951 | Japan | 17–145 | New Zealand | Kombe la dunia la raga kundi C | 17,000 |
Kombe la mataifa Afrika ya 1996
haririUwanja wa michezo wa Free state ilikuwa miongoni mwa viwanja vilivyotumika kwa kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 1996. Mechi ya makundi sita(6) na mechi ya robo fainali zilichezwa katika uwanja huu.
Tarehe | Muda (SAST) | Timu #1 | Matokeo | Timu #2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
14 Januari 1996 | Zambia | 0–0 | Algeria | Kundi B | 9,000 | |
15 Januari 1996 | Sierra Leone | 2–1 | Burkina Faso | Kundi B | 1,500 | |
18 Januari 1996 | Algeria | 2–0 | Sierra Leone | Kundi B | 1,500 | |
20 Januari 1996 | Zambia | 5–1 | Burkina Faso | Kundi B | 2,000 | |
24 Januari 1996 | Zambia | 4–0 | Sierra Leone | Kundi B | 200 | |
25 Januari 1996 | Ghana | 2–0 | Msumbiji | kundi D | 3,500 | |
27 Januari 1996 | Zambia | 3–1 | Misri | Robo fainali | 8,500 |
Kombe la shirikisho la FIFA ya mwaka 2009
haririUwanja wa Free state ulikuwa moja wapo ya viwanja vilivyotumika kwa michezo ya shirikisho la FIFA ya mwaka 2009.
Tarehe | Muda (SAST) | Timu #1 | Matokeo | Timu #2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
15 Juni 2009 | 16:00 | Brazil | 4–3 | Misri | Kundi B | 27,851 |
17 Juni 2009 | 16:00 | Hispania | 1–0 | Iraq | Kundi A | 30,512 |
20 Juni 2009 | 20:30 | Hispania | 2–0 | Afrika Kusini | Kundi A | 38,212 |
24 Juni 2009 | 20:30 | Hispania | 0–2 | Marekani | Nusu fainali | 35,369 |
Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010
haririKabla ya kombe la dunia la FIFA mwaka 2010, upanuzi wa kwanza ulifanyika katika upande wa magharibi mwa uwanja na kuongeza uwezo wa kubeba mashabiki kutokea 36,538 hadi 40,911.[1]
Bloemfontein walipokea kiasi cha fedha R221 milioni kwa ajili ya kuboresha uwanja. Japo makadirio ya fedha yalikuwa R245 milioni, jiji liliamua kufidia kiasi kilichobaki.[2] Zabuni zilitangazwa mwezi Februari na Machi mwaka 2007. Maboresho yalianza Julai 2007.[3]
Tarehe | Muda (SAST) | Timu #1 | Matokeo | Timu #2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
14 Juni 2010 | 16.00 | Japan | 1–0 | Kamerun | Kundi E | 30,620 |
17 Juni 2010 | 16.00 | Ugiriki | 2–1 | Nigeria | Kundi B | 31,593 |
20 Juni 2010 | 13.30 | Slovakia | 0–2 | Paraguay | Kundi F | 26,643 |
22 Juni 2010 | 16.00 | Ufaransa | 1–2 | Afrika Kusini | Kundi A | 39,415 |
25 Juni 2010 | 20.30 | Switzerland | 0–0 | [[Image:|22x20px|border|Bendera ya Honduras]] Honduras | Kundi H | 28,042 |
27 Juni 2010 | 16.00 | Ujerumani | 4–1 | Uingereza | Mzunguko wa 16 | 40,510 |
Marejeo
hariri- ↑ "fussballtemple". Fussballtempel.net. Iliwekwa mnamo 2010-06-17.
- ↑ "Sunday Times". Sunday Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-14. Iliwekwa mnamo 2010-06-17.
- ↑ "Official upgrade progress report as at May 2008" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-07-27. Iliwekwa mnamo 2010-06-17.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Free State kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |