Vendemiale (alifariki 483) alikuwa askofu wa Gafsa (leo nchini Tunisia) hadi alipopelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Corsica (leo nchini Ufaransa) kutokana na dhuluma za Wavandali Waario dhidi ya Wakatoliki. Ilikuwa vilevile kwa maaskofu wengine 650.

Baada ya kuinjilisha kisiwa hicho pamoja na maaskofu Eujeni wa Karthago na Lonjino wa Pamaria, aliendelea hata nje yake. Hatimaye alifia dini kwa kukatwa kichwa kwa amri ya mfalme Huneriki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Mei[1][2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  2. https://catholicsaints.info/saint-vindemialis-of-africa/
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.