Korsika
Korsika (kwa Kifaransa:Corse; kwa Kikorsika: Corsica) ni kisiwa cha Ufaransa katika Mediteranea. Ni kisiwa kikubwa cha nne katika Mediteranea baada ya Sisilia, Sardinia na Kupri.
Korsika | |||
| |||
Nchi | Ufaransa | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Ajaccio | ||
Eneo | |||
- Jumla | 278,650 km² | ||
Tovuti: http://www.corse.fr/ |
Iko upande wa kusini kwa Ufaransa na upande wa magharibi kwa Italia bara (lakini kaskazini kwa kisiwa chake cha Sardinia). Umbali wa bara ni kilomita 90 hadi Italia na kilomita 170 hadi Ufaransa kusini. Umbali na Sardinia ni kilomita 11 pekee.
Kisiwa kina pwani yenye urefu wa kilomita 1,000 na milima mingi inayofikia kimo cha mita 2706.
Wilaya ni Corse-du-Sud na Haute-Corse.
Katika historia kisiwa kilikuwa chini ya Genua tangu mwaka 1300 hadi karne ya 18 kilipouzwa kwa Ufaransa na hivyo kuwa sehemu ya jirani ya kaskazini.
Hata utamaduni wa watu wa Korsika ulikuwa karibu zaidi na Italia kuliko Ufaransa. Lugha ya Kikorsika iko karibu na lahaja za Italia. Lakini leo hii ni takriban asilimia 35 tu za wakazi wanaotumia lugha hii. Serikali ya Ufaransa iliwahi kupigia marufuku matumizi yake shuleni lakini tangu mwaka 1989 imekubaliwa kama lugha rasmi pamoja na Kifaransa.
Eneo la kisiwa ni km² 8680 zinazokaliwa na wakazi 278,650.
Mwenyeji mashuhuri kabisa wa Korsika alikuwa Napoléon Bonaparte.
Miji muhimu ni (majina ya Kikorsika)
Viungo vya nje
hariri- Corsica travel guide kutoka Wikisafiri
- PhotoGlobe - Corsica A collection of photos of Corsica together with GPS-based positions
- CNN Ilihifadhiwa 8 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine. CNN coverage of rejection of autonomy proposals in 2003
- University of Corsica
Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Korsika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |