Verano wa Vence
Verano wa Vence (alifariki 480 hivi) alikuwa askofu wa 4 wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa).
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[1].
Maisha
haririKisha kufiwa mama yake Galla, alitawa pamoja na baba yake, Eukeri wa Lyon, na ndugu yake Saloni katika monasteri ya Lérins, iliyoanzishwa na Honorati wa Arles juu ya kisiwa karibu na Antibes[2].
Kutokana na sifa yake, baba yake alichaguliwa kuwa askofu wa Lyon mwaka 434 hivi akaendelea na cheo hicho hadi kifo chake.
Hapo Verano alishika nafasi yake[3] , na Saloni akawa askofu wa Geneva.
Verano alimuandikia Papa Leo I kumshukuru kwa jinsi alivyotetea imani sahihi kuhusu Neno alivyofanyika mtu katika barua kwa Flaviano wa Kostantinopoli [4].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Gregori wa Tours, Historia Francorum (The History of the Franks) (London, England: Penguin Books, Ltd., 1974).
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |