Eukeri wa Lyon (380 hivi - 449 hivi) alikuwa askofu mkuu wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa)[1].

Sanamu ya Eukeri wa Lyon.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Novemba[2].

Maisha na maandishi hariri

Kisha kufiwa mke wake Galla, alitawa pamoja na wanae Veranius and Salonius katika monasteri ya Lérins, iliyoanzishwa na Honoratus juu ya kisiwa karibu na Antibes.

Baadaye alihamia kisiwa cha Lerona (sasa Sainte-Marguerite), akisoma na kujitesa kwa lengo la kujiunga na Mababu wa jangwani.

Kumbe Yohane Kasiano alifika huko Marseille na kuandika sehemu ya pili ya Collationes (namba 11-17) kwa heshima ya Eukeri na Honoratus.

Wakati huohuo Eukeri aliandika De laude Eremi ("Sifa ya Jangwa") kwa askofu Hilari wa Arles.[3]

Pia aliandika Epistola paraenetica ad Valerianum cognatum, de contemptu mundi kuhusu kudharau ulimwengu.

Liber formularum spiritalis intelligentiae inatetea uhalali wa kufafanua kiroho Biblia.

Kati ya maandishi yake kuna pia Institutiones ad Salonium, barua na homilia kadhaa n.k.

Kutokana na sifa yake, alichaguliwa kuwa askofu wa Lyon mwaka 434 hivi; kwa msingi huo hakika alihudhuria Mtaguso wa Orange (441) akaendelea na cheo hicho hadi kifo chake.[3]

Hapo mwanae Veranus alishika nafasi yake, na mwanae mwingine, Salonius, akawa askofu wa Geneva.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Salvator Pricoco, 1965. Eucherii De Laude eremi (University of Catania) This edition establishes the best, most recent Latin text.
  • Bishop of Tours Gregory, Historia Francorum (The History of the Franks) (London, England: Penguin Books, Ltd., 1974).
  • Ford Mommaerts-Browne, "A Speculation", http://archiver.rootsweb.ancestry.com/th/read/GEN-ANCIENT/2004-03/1079586413 Archived 13 Februari 2015 at the Wayback Machine..
  • Sidonius Apollinaris, The Letters of Sidonius (Oxford: Clarendon, 1915) (orig.), pp. clx-clxxxiii; List of Correspondents, Notes, V.ix.1.
  • K. Pollmann, "Poetry and Suffering: Metrical Paraphrases of Eucherius of Lyons’ Passio Acaunensium Martyrum," in Willemien Otten and Karla Pollmann (eds), Poetry and Exegesis in Premodern Latin Christianity: The Encounter between Classical and Christian Strategies of Interpretation (Leiden and Boston: Brill, 2007) (Supplements to Vigiliae Christianae, 87).

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.