Vinsenti alikuwa shemasi wa jimbo la Zaragoza, Hispania.

Picha yake iliyochorwa na msanii Tomas Giner (1462-1466).

Mzaliwa wa Huesca, wakati wa dhuluma ya Kaisari Dioklesian dhidi ya Wakristo, alifungwa na kuachwa bila chakula, akateswa vikali sana, akafa kwa ajili ya dini yake huko Valencia mwaka 304.

Heshima ya watu kwake kama mtakatifu ilienea haraka sana katika Kanisa lote.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Januari[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.