Visiwa vya Kamanda

Visiwa vya Kamanda (pia "Komandorski", Kirusi: Командорские острова komandorskiye ostrova) ni kundi la visiwa katika Bahari ya Bering, takriban kilomita 200 - 300 upande wa mashariki wa Rasi ya Kamchatka katika Siberia, upande wa mashariki mwa Urusi.

Ramani ya Kirusi ya Visiwa vya Kamanda
Kijiji cha Nikolskoye kwenye Kisiwa cha Bering ni makao makuu ya wilaya ya Komadorski

Zinahesabiwa kuwa sehemu ya magharibi kabisa ya pinde la Visiwa vya Aleuti. Umbali hadi kisiwa cha karibu cha Aleuti ni mnamo kilomita 333.

Kuna visiwa viwili vikubwa zaidi ambavyo ni Kisiwa cha Bering na Kisiwa cha Medny pamoja takriban visiwa 14 vidogo zaidi. Jumla ya eneo la nchi kavu ni mnamo km2 1660.

Visiwa hivyo havina miti kutokana na hali ya hewa ambayo ni baridi mno pamoja na kuwa na upepo mkali, ukungu mzito na mitetemeko ya ardhi.

Wakazi wote waliopo hukaa kwenye Kisiwa cha Bering penye kijiji kimoja cha wavuvi, ambao idadi yao haizidi watu 800 hivi.

Visiwa hivi viligunduliwa na kamanda Vitus Bering kwenye mwaka 1741 aliporudi kutoka safari yake ya kufika Alaska. Bering alifariki dunia kwenye kisiwa kilichopokea baadaye jina lake.

Visiwa hivyo kwa jumla vimeteuliwa kama hifadhi ya bioanwai kutokana na wingi wa viumbehai vya baharini na ndege.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kulitokea mapigano ya manowari za Marekani na Japani takriban kilomita 100 upande wa kusini wa visiwa hivyo.

Picha zote ni za Kisiwa cha Bering

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Kamanda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.