Vita Kuu ya Dunia ni jina linalotumika kwa ajili ya vita inayohusu nchi nyingi katika sehemu mbalimbali za dunia badala ya eneo la nchi kadhaa pekee.

Kwa kawaida vita mbili za karne ya 20 huitwa "Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia" (1914-1918) na "Vita Kuu ya Pili ya Dunia" (1939-1945).

Jina hilo limepatikana tangu mwanzo wa karne ya 20 katika miaka kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ilipoonekana ya kwamba vita ikianzishwa itahusu sehemu kubwa ya dunia kutokana na mapatano kati ya mataifa makubwa ya Ulaya yaliyotawala nchi nyingi duniani chini ya mfumo wa ukoloni.

Wanahistoria wengine hudai ya kwamba hali halisi vita kuu ya kwanza ilizohusu dunia yote ilikuwa vita ya miaka saba (1756-1763) kati ya Uingereza na madola ya Kijerumani ya Uprusi na Hannover dhidi ya Ufaransa, Urusi, Austria, Uswidi, Saksonia na Hispania. Mapigano yalitokea Ulaya, Amerika ya Kaskazini, Visiwa vya Karibi, India, Asia ya Mashariki, Afrika na baharini kote duniani.

Viungo vya nje

hariri